Na Editha Karlo wa michuzi Tv,Kigoma

WAZAZI na walezi Mkoani Kigoma wametakiwa kushiriki ipasavyo kwa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya kwaajili ya kupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa ya surua,Rubella na Polio.

Hayo ameyasema na katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Rashid Mchatta kwenye mafunzo kwa wanahabari na wataalam wa afya kwaniaba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga amesema chanjo hizo ni muhimu kwa watoto hivyo ni wajibu wa kila mzazi na mlezi kuhakikisha watoto wanapata chanjo hizo.

Alisema chanjo hizo ni salama na zinalenga kuwakinga na kuwasaidia watoto kuepukana na maradhi hayo wananchi wasisikilize uvumi wowote unaoweza kujitokeza wa upotoshwaji wa umma juu ya huduma hiyo.

Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote alisema kuwa jumla ya watoto 422,424 wenye umri wa miezi 6 mpaka miezi 59 watapatiwa chanjo ya surua na Rubella pamoja idadi ya watoto 201,800 wenye umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi mwaka mmoja na nusu watapatiwa chanjo ya polio.

Dkt Chawote amesema kampeni ya hiyo inatajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 26 na kukamilika tarehe 30 septemba mwaka huu.




"Zoezi hili la kuwapatia watoto chanjo litafanyika kwenye vituo mbalimbali katika halmashauri zetu zote za Mkoa wa Kigoma,hivyo naiomba jamii itoe ushirikiano wa kutosha ili tuweze kupata matokeo chanja ya kufikia malengo tuliyokusudia ya kuwafikia watoto wote waliolengwa kupatiwa chanjo hizo"alisema Dkt Chawote

Mratibu wa chanjo Mkoa wa Kigoma Kulwa Makono amesema kuwa hilo ni zoezi la Dunia nzima na Kitaifa kupambana na magonjwa kwa watoto.
"Zoezi hili siyo la Mkoa wa Kigoma pekee ni zoezi linalofanyika Dunia nzima na Kitaifa pia hivyo wazazi wajitokeze kwa wingi kuleta watoto wao waweze kupatiwa chanjo hizo"alisema

Makono alisema kuwa ugonjwa wa surua na Rubella yanaambukizwa kwa njia ya hewa kwa upande wa polio ni kwa njia ya kula au kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye vijidudu vya polio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...