Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Ifakara na Kilombero (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini.

Watumishi wa umma wa Halmashauri ya Mji Ifakara na Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo wilayani humo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini..


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (aliyesimama) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Ifakara na Kilombero (pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini.

……………..

Na. Aaron Mrikaria

Watumishi wa umma wanaofanyakazi makao makuu ya Halmashauri za Wilaya nchini wametakiwa kutofanyakazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia weledi, ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia na watumishi wenzao wanaotoka pembezoni kufuata huduma wilayani.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri za Wilaya ya Kilombero,Ifakara Mji na Malinyi kwa nyakati tofauti, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini.

Dkt. Ndumbaro amewasisitiza watumishi hao, kuhakikisha wanawahudumia vizuri watumishi wa umma wanaotoka kwenye kata, tarafa na vijiji ili nao waweze kuwahudumia vizuri wananchi katika maeneo yao ya kazi.

“Hatuna budi kuwahudumia ipasavyo wananchi na watumishi wanaotumia gharama zao kufuata huduma wilayani sanjari na kupoteza muda wao, tusiwaache waondoke bila kupata huduma inayostahili” amesema Dkt. Ndumbaro.

Aidha Dkt. NDUMBARO amewashauri watumishi wanaotaka kusoma shadada ya pili wabobee katika fani zinazoendana na shahada ya kwanza kwakuwa shahada ya kwanza ndio msingi wa taaluma walizonazo, na endapo mtumishi atajiendeleza kwa kuchukua shahada ya pili tofauti na ya kwanza atakuwa amejiendeleza katika kada tofauti hivyo kukosa fursa ya kubadilishiwa cheo (recategorization) na kukosa sifa ya kupata kibali cha mshahara binafsi.

Dkt. Ndumbaro amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri za Wilaya ya Kilombero, Ifakara Mji na Malinyi kuhimiza uwajibikaji, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) aliyemtaka kuchunguza weledi wa utendaji kazi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...