Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

WAZEE wametakiwa kutoa nafasi kwa vijana kugombea katika nafasi za uongozi, kuacha tabia ya kuwatisha na kuwazuia vijana ili kuwajengea msingi mzuri ikwemo kuwapima katika nafasi mbali mbali ili kuweza kujenga viongozi watakao ongoza kwa hekima na busara.

Rai hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James Mkoani Kigoma wakati wa uzinduzi wa Oparesheni ya Kigoma ya Kijani , alisema Nchi inahitaji utayari wa vijana na uongozi wa vijana hivyo lazima wazeee wawaachie vijana kugombea na wasiwanyime nafasi iliwaweze kuwapima na kuwajengea weredi wa uongozi na busara kwa kipindi hiki ambacho bado kunawazee wenye busara iliwaweze kuwapa bisara hizo na waweze kubaki viongozi wazuri.

Alisema Vijana wakipewa nafasi kwa kipindi hiki ambacho bado kuna wazee wa kuwapima kutokana na busara zao namna gani ya kuongoza, itasaidia kutengeneza Taifa lenye uongozi ulio bora na unaozingatia misingi ya waasisis wa Taifa la Tanzania na kuepuka kuacha taifa la watu wanaofanya maamuzi bila kutumia busara.

Sambamba na hilo James aliwataka Wananchi wa mkoa wa Kigoma kuwapuuza wanasiasa wanaotumiwa na watu wa Nje kuivuruga Nchi, kwa kusema kwamba Tanzania kunamatatizo na hakuna kilichofanyika jambo ambalo sio kweli kwa kuwa mambo yaliyofanywa na Serikali iliypo madarakani yanaonekana .

Alisema Siasa hazifai kutweza juhudi zinazofanywa na serikali kwa maslahi ya Taifa letu hivyo wanasiasa wanatakiwa kujua kazi yao ni kukosoa pale jambo linapoonekana haliendi sawa na kupongeza pale serikali inapofanya vizuri na sio kutumiwa na watu wa Nje kuwakatisha tamaa viongozi wanaoifanya Nchi isongembele kwa kuwa uchumi ukikua ni wawatanzania wote na ajira zikipatikna ni kwa wote kwa kuwa nchi hii imejengwa kwa uzalendo na Usawa. 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma, Amandus Nzamba alisema watajitahidi kutoa nafasi kwa vijana, ili na wao waweze kujifunza namna ya kuongoza na kuiletea nchi maemdeleo.

Aidha aliwaomba vijana kujitokeza kwa wingi kugombea uongozi kuanzia ngazi ya serikali za mitaa hadi uongozi wa juu, kwa kuwa vijana wengi wanaogopa kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali hivyo sasa ni wakati wao.

Nae katibu wa Umoja wa Vijana(UVCCM) kigoma Rashidi Semindu alisema Vijana Kigoma wamejipanga katika Chaguzi zinazokuja ikiwa ni pamoja na kulirudisha jimbo la kigoma mjini kwa chama cha mapinduzi na kuhakikisha vijana wote wanajitokeza na kupambana na upinzani kwa Mkoa wa Kigoma.

Alisema wamefanikiwa kuwarudisha kwenye chama cha mapinduzi vijana 82 wakiwemo waliokuwa Viongozi wa chama cha ACT wazarendo, wataendelea kuwashawishi Vijana kutokana na mambo Makubwa yanayofanywa na viongozi wa CCM Kwa kuleta maendeleo Tanzania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM)Taifa Kheri James pembeni ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kigoma Silvia Sigula akikaribishwa na Vijana wa umoja huo Mkoani kigoma jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...