WWAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema kuwa Tamasha la utamaduni na sanaa la nchini za Afrika mashariki litumike kukiuza kiswahili ili na nchini mwanachama wa Afrika mashariki waweze waongee lugha hii adhimu ambayo sasa ni lugha rasmi katika jumuiya za Afrika.
Amesema hayo alipotembelea maonesho ya Tamasha la Uatamaduni na Sanaa la nchi za Afrika amashariki al-maalufu kama JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwa nja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
"Nimetembelea mabanda mbalimbali na kujionea bidhaa mbalimbali za asili na utamaduni wa maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki za wajasiriamali wa nchi zote".
Amesema kuwa wizara ya Tamisemi ni chumvi, Afya, elimu vipo chini ya wizara yake, lakini wizara ya habari utamaduni, Sanaa na Michezo hususani Maafisa Utamaduni wa Mikoa,Wilaya na Halmashauri wako TAMISEMI,hivyo unaweza kuona kwanini yupo hapa.
Hata amewapongeza wizara ya habari na utamaduni kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuhakikisha tamasha hili linafanyika kama lilivyopangwa na kwa mafanikio makubwa hasa kukidhi kiu ya wananchi wanaohudhuria tamasha hili adhimu.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akimsikiliza mkuu wa kikundi cha kukuna nazi ikiwa washiriki ni washindi katika makundi mbalimbali walioshindanishwa kukuna nazi. Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST.Ikiwa wamepata washindi wa tatu kutoka makundi tiofauti wakiwa wananwake wawili pamoja na mwananume mmoja.
Washiriki wa kukuna nazi wakisubiri filimbi ipigwe katika mashindano ya kukuna nazi wakiwa na kipimo cha ulaini wa nanzi pamoja na atakayewahi kumaliza na ikiwa safi. Washiriki ni washindi katika makundi mbalimbali walioshindanishwa kukuna nazi. Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST.
Washiriki wa mchezo wa kusuka ukiri wakicheza mchezo wao wa asili kusuka ukili. Hii ni katika Tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akiangalia jinsi wasuka ukili walivyofanikiwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia ukili. Hii ni katikaTamasha la JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST.
Mambo ya Utamaduni yakioneshwa. Hapa ni Mishale na Mikuki.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akiangalia meza na viti vilivyotengenezwa na Mianzi. Yote hayo ni katika tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taiafa jijini Dar es Salaam.
Utamaduni na sanaa ya Matanzania.
Mambo ya utamaduni kutoka Burundi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...