NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Bagamoyo Mkoani Pwani, limeiasa Jumuiya  ya Maridhiano wilayani humo kuacha kuingilia mamlaka nyingine ambazo zipo kisheria na badala yake zitekeleze majukumu yao ya kikazi  .

Baadhi ya madiwani akiwemo, diwani wa kata ya Fukayose ambae pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo Ally Issa, waliyasema hao wakati wa baraza lililowakaribisha viongozi wa Jumuia hiyo, kwa lengo la kuwatambua na kufahamu mipaka ya kazi zao.

Aidha inadawa waliwahi kufika ndani ya kata ya Fukayose kuhoji taarifa ya mapato na matumizi, jambo ambalo ni kinyume na malengo ya Jumuiya inayolenga usuluhishi na kuweka sawa mambo pale penye migongano.

Nae diwani wa kata ya Yombo Mohammed Usinga, alisema baadhi ya viongozi hao wanatekeleza mambo nje ya taratibu kwani wamekuwa wakifika katika ofisi ya kata na kumtaka mtendaji kutoka nje ya ofisi ili wafanye mkutano.

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Dauson Shigea alisema Jumuiya hiyo imesajiliwa kisheria na inafanya kazi ya maridhiano na wanaikana kamati ya amani kutokana na kwamba haipo.

Akitoa ufafanuzi huo, juu ya mkanganyiko wa kushahabiana majukumu ya kazi baina ya jumuiya ya maridhiano na kamati ya amani, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Zainab Kawawa alisema ,kamati hiyo ipo na inafanya kazi kwa mujibu wa taratibu kitaifa,kimkoa na kiwilaya.

Zainab alikemea asitokee mtu ,kundi la watu ,Jumuiya ama taasisi yeyote kupotosha na kuvumisha kuwa kamati ya amani imekufa kwa maslahi binafsi.

"Nilishapokea taarifa pia zisizo rasmi kuwa wilayani humo kuna Jumuiya ya maridhiano na yeye bado sijaifahamu na kimsingi inafanyaje kazi zak".

Nae Katibu wa BAKWATA wilaya ya Bagamoyo ,ambae pia ni mratibu wa kamati ya amani wilayani humo, Hashim Juma alipoulizwa kuhusu kufutwa kwa kamati hiyo alisema hana taarifa hizo kwani endapo hatua hizo zingechukuliwa wangepewa taarifa za kimaandishi kutoka ngazi ya kitaifa na kimkoa.
  Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Zainab Kawawa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...