Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Kampuni ya Mawakili ya AVIS Legal imeandaa kampeni ya kutoa elimu dhidi ya ukatili kwa Wanawake na Watoto katika Manispaa Ilala jijini Dar es Salaam.

Kampeni hiyo imeshirikisha walimbwende mbalimbali ambapo watakwenda kutoa elimu kuhusiana na ukatili ikiwemo kutoa msaada kisheria familia zilipitiwa na ukatili.

Akizungumza na waandishi Wakili wa AVIS Legal Henry Mwinuka kutokana na takwimu za ukatili kwa wanawake na watoto wameona wanawajibu wa kutoa elimu ya ufahamu juu ya matendo ya ukatiliwa wa aina yeyote unaoendelea nchini.

Amesema kampeni hiyo sambamba na ajenda ya mwaka 2030 ya malengo ya maendeleo yasiyo na ukomo na pia ajenda ya kamisheni umoja wa Afrika 2063 yenye dhima ya Afrika tunayoitaka kwa kuweka mazingira salama kwa watoto wote kuishi na kutokomeza kabisa ukatili dhidi ya watoto na wanawake.

Mwinuka amesema kwa muda mrefu vitendo vya ukatili wa dhidi ya wanawake na watoto vimekuwa vikiendelea kushamiri na hivyo kuhatarisha mstakabali mwema wa kujenga jamii yenye kujali usawa na haki.

Amesema Takwimu 2015/2018 zinaonyesha ongezeko kubwa na kuendelea kushamiri kwa vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ambavyo vimeathiri maisha yao na kukiuka haki za binadamu.

Nae Wakili Hamza Jabir amesema kampeni hiyo ni ya kujitolea hivyo watu wanaotaka wanaweza kuungana katika kujenga jamii isiyo na ukatili

Amesema kuwa wanaanza na Wilaya ya Ilala ambapo watapata picha na kuweza kuifanya kampeni hiyo nchi nzima kwani ukatili uko wa aina tofauti tofauti kwa watoto na wanawake.
Wakili wa AVIS Legal Henry Mwinuka akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kampeni ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto inayotarajiwa kuanza katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Wakili Hamza Jabir akitoa maelezo kuhusiana na kampeni ya ukatili wa Wanawake na watoto itakayoanza katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Mwilimbwende na Wakili Anita Mlay akitoa namna atavyotoa elimu katika kampeni ya ukatili wa Wanawake na watoto itakayoanza katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...