Picha ikionyesha wa kwanza kushoto mkurugenzi wa ununuzi na ugavi wa benki ya CRDB Pendason Philemon akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 iliotolewa na benki ya CRDB kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanawake chuoni hapo , kwanza kulia kaimu mkuu wa chuo cha polisi moshi SACP Gemini Mushy hafya iliyofanyika chuoni hapo. Picha na Woinde Shizza
Na Woinde Shizza Michuzi TV, Kilimanjaro
Kufuatia changamoto kubwa ya uchakavu wa vyoo vya askari wanafunzi wa kike
katika chuo cha polisi moshi (CCP) ambayo imekuwa ikihatarisha afya ya wanafunzi
hao wawepo chuoni hapo benki ya CRDB imetoa kiasi cha shilingi milioni kumi
kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo vya chuo hicho ili kuwapunguzia adha hiyo
wanafunzi wa kike.
Msaada huo unakuja wakati mwafaka kutokana na chuo hicho kuwa na majengo ya
muda mrefu akikabidhi msaada huo mkurugenzi wa ununuzi na ugavi wa
benki ya CRDB Pendason Philemon amesema msaada huo ni moja ya sera maalum
iliyojiwekea ya benki hiyo ya kusaidia jamii yenye kuagiza na kuelekeza
kutenga asilimia moja ya faida yake kila mwaka.
“Dhamira hii ya kusaidia jamii kunaifanya benki ya CRDB kuendelea kuwa mdau
wa maendeleo kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa jamii inayotuzunguka pamoja na
kusaidia serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania katika jitihada zake
za kupeleka huduma za kijamii zenye kukidhi mahitaji ya wananchi hususani
katika kuliunga mkono jeshi la polisi katika jitihada zake za kulinda
wananchi na mali zao.”alisema Philemon.
Alisema benki ya CRDB inafahamu fika kuwa vyoo ni afya na usafi katika
maisha ya binadamu yoyote yule duniani hivyo basi waliposikia chuoni
hapo na kukuta
kina uhitaji wa ujenzi na maborsho ya vyoo vya wananwake hawakusita
kama benki kuunga mkono ombi hilo ili kuwezesha ujenzi huo.
Awali Gemini Mushy kaimu mkuu wa chuo cha polisi Moshi alisema msaada huo
uliotolewa na Benki ya CRDB ni muhimu kwa kuwajengea Askari polisi
mindombinu bora ambapo licha ya kutumia bajeti ya serikali bado wamekuwa
wakikabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundo mbinu chuoni hapo kufuatia
majengo hayo kuwa ya muda mrefu.
“Ni ombi letu pia katika mipango yenu kuzidi kuangalia mtakavyoweza kutia
shime ili kuborsha mazingira ya kuwafundishia askari wetu ili watokapo hapa
wawe na ari kubwa Zaidi ya kuwalinda raia na mali zao kwa ufanisi Zaidi ili
pato binafsi la mtanzania liweze kukua Zaidi na utashi wa kuwekeza kupitia
CRDB uweze kukua sawia”alisema SACP MUSHY
Kwa upande wake meneja wa benki ya CRDB kanda ya kaskazini Chiku Issa
alisema CRDB iliguswa na hali mbaya ya vyoo vya wanachuo wa kike hivyo
kuamua kuasaidia kutatua changamoto hiyo.
“Mimi kama mama kwa kweli nilipofika hapa baada ya kupokea maombi kwa mmoja
wa wadau ambae ni mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka niliguswa na kwa
kutambua kauli mbiu ya choo ni nyumba niliona ipo haja ya kuwasaidia
askari wetu ambao ndio walinzi wa mali zetu na raia” alibainisha Chiku.
Nae mlezi wa wanafunzi wa kike na mkufunzi katika shule ya polisi Tanzania
mrakibu mwandamizi wa jeshi la polisi Pili Misungwi ameshukuru benki hiyo
kwa msaada huo ambao amesema wanaishukuru benki hiyo kwa wepesi na uharaka
wa nanma walivyolishughulikia suala hilo ambalo lilikuwa ni changamoto
kubwa kwa wanafunzi askari wa kike.
“Tulihusisha wadau mbali mbali lakini mmoja wa wadau waliojitokeza kwa
haraka na kuamua kutusaidia ni CRDB kwa kwa kweli kwa niaba ya mkuu wa
jeshi la polisi nchini na mkuu wa chuo tunaishukuru sana CRDB kwa kutambua
umuhumu wa kusaidia askari wanafunzi wa kike kwa sababu maumbile ya kike na
kiume ni tofauti kwa kuwa watoto wa kike ni rahisi sana kupatwa na magonjwa
endapo mindombinu haitakuwa misafi”alisema SSP Misungwi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...