Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Msanii wa Kizazi kipya nchini, Rajabu al maarufu kwa jina la Harmonize ametambulisha kibao chake kipya cha UNO kwa wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam ikiwa ni kwa mara ya kwanza kujitokeza kwa mashabiki wake tangu ajitoe kwenye Kundi la Wasafi.

Harmonize katika utambulisho huo amesindikizwa na Wasanii wa Bongo Fleva na Wasanii wa Hip Hop pamoja na Wasanii wa mziki wa Singeli wakiwakilishwa na Msanii maruufu wa miondoko hiyo ya Singeli, Mzee wa Bwax.

Harmonize amedai miaka minne iliyopita alifika jijini Dar es Salaam ambapo alifikia eneo la Mzinga, Mbagala akitokea nyumbani kwao Mtwara, amesema kabla yakuanza kuimba alifanya kazi yakuuza Mitumba kabla yakujiunga na Kundi la WCB Wasafi.

Katika utambulisho huo, Msanii aliyewahi kutamba na Wimbo wa Mpenzi wangu Bubu, H BABA amemtunuku Tuzo ya heshima, Harmonize baada yakutambua mchango wake kwenye mziki kwa kumtaja kwenye kibao chake.

Hata hivyo, Harmonize ameomba kura kwa mashabiki wake katika Tuzo za MTV EUROPEAN MUSIC AWAARDS 2019 katika Kipengele cha Best African Act zitakazotolewa hivi karibuni wakati yeye akiwa ni mmoja wa Wasanii wanaowania tuzo hizo.

Pia, Harmonize ameahidi kwa mashabiki wake kuwa atafanya 'Show' kama hiyo, Desemba 25 ya mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...