Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo amesema kuwa Bonanza la Michezo litaendelea kufanyika kila baada ya miezi miwili na litahusisha michezo mbalimbali.

Bw.Singo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipozungumza wakati akishukuru Watumishi wa Serikali na wananchi wa Jijini la Dodoma waliojitokeza kushiriki Bonanza hilo.

“Bonanza hili litafanyika kila baada ya miezi miwili lengo ikiwa ni kuimarisha afya zetu pamoja na kuimarisha upendo,amani na mshikamano tulionao Tanzania”alisema Bw.Singo.

Aidha Bw.Singo amesema kuwa Bonanza hilo litashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mbio za taratibu,mazoezi ya viungo, mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na michezo mingine.

Naye Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Bw.Daudi Manongi amesema kuwa Bonanza hilo limekuwa na faida nyingi kwani limewakutunisha Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Jiji la Dodoma katika kuimarisha afya zao na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza kazi zao.

Katika bonanza hilo timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya habari,Elimu na timu ya Joggin kutoka Dodoma ziliibuka washindi ,huku timu ya mpira wa miguu ya Serikali ikiifunga magoli matatu timu ya Boabao Queens ya Jiji la Dodoma iliyoambulia goli moja.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.
Muongozaji wa mazoezi Bw.Simba akiongoza mazeozi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.


Baadhi ya Watumishi wa Serikali na wananchi wa jiji la Dodoma wakifanya mazeozi ya viungo wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.
4.Timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ikiwa uwanjani ikishindana na timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo timu hiyo iliibuka kidedea katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara hiyo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma.
Timu za Mpira wa miguu za Serikali na Baobao Queens ya Jijini Dodoma zikichuana vikali katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo lililofanyika leo katika Uwanja Jamhuri Jijini Dodoma ambapo timu ya Serikali ilishinda kwa magoli matatu dhidi ya goli moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...