Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) imejiwekea malengo ya kufikia Kiasi cha Shilling Bilioni 12 kwa mwezi katika makusanyo ya ankara za maji kwa wateja wake Dar es Salaam na Pwani.

Ndani ya Mwaka mmoja Dawasa wameweza kuongeza ukusanyaji wa ankara za maji kwa kukusanya Shilingi Bilioni 11. 11 mwezi Septemba mwakaa hu.

Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja, Ritamarry Lwabulinda amesema kabla ya  kuunganishwa kuwa Dawasa moja, Makusanyo ya mwezi Agosti mwaka jana ankara za maji kwa mwezi yalikuwa Bilioni 9.2.

Amesema, kiwango cha mapato ya ndani ya mwaka mmoja wa Dawasa kimekuwa kutoka wastani wa makusanyo ya Sh. Bil 9.2 kwa mwezi hadi sasa wanakusanya wastani wa Sh. Bil. 11 kwa mwezi.

“Kwa mwaka wa fedha uliokwisha Dawasa ilikusanya Sh. Bil. 135 sawa na asilimia 95 ya lengo” alisema

Ritamarry amesema kuongezeka kwa mapato ndani ya mamlaka yanatokana na wateja ambao ni waaminifu, kudhibiti mivujo na mamlaka kuzidi kutanua wigo wa utoaji huduma kwa wateja wa zamani na wapya.

"Upotevu wa maji umepungua kwa asilimia kubwa ambapk mwaka 2015 upotevu ulikuwa asilimia 53 na Shirika la DAWASCO ilikuwa inakusanya kiasi cha Tsh Bil 3.2 kwa mwezi ila kwa sasa hali ya upatikanaji maji Jijini imepanda hadi asilimia 85 na kwa mwezi wa Agosti mwaka huu upotevu umefikia asilimia 39 ya kiwango cha Maji yasiyolipiwa," amesema.

 Amesema anawashukuru wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha na Bagamoyo kwa mwitikio wao kwenye kulipa bili zao kwa wakati na hata wale wenye malimbikizo pia wameweza kupunguza jambo lilifanya kupanda kwa makusanyo kwa mwezi. 

"Kwa sasa  Dawasa inatekeleza miradi zaidi ya 40 kwa pesa za ndani ambapo ni asilimia 35 ya mapato ya kila mwezi, hivyo kupanda kwa makusanyo kutaiwezesha mamlaka hiyo kutekeleza miradi ya maji mingi zaidi itakayowezesha kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji,"

Ameongeza kuwa kwa upande wa huduma kwa wateja imefanikiwa kuboresha namna ya ulipaji wa Ankara. “wateja wetu wamerahisishiwa namna ya ulipaji wa ankara za maji kupitia mtandao, hiyo imewarahisishia wananchi kulipia huduma na  wamekuwa wakikumbushwa mara kwa mara njia za malipo ili kuweza kulipa kwa wakati huduma muhimu ya Maji.

Mpendwa Mteja, tunakushukuru kwa kulipia bili yako ya September kwa wakati, Umeiwezesha DAWASA kukusanya Tshs.11.11 Billion. Ahsante sana, Tunakusihi kuendeelea kulipia Bill zako Kwa wakati. Piga (0800110064)," Taarifa ya Dawasa kwa wateja wake.
Afisa Mtendaji Mku wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa pongezi kwa baadhi ya wafanyakazj waliofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia malengo ya kukusanya Bilioni 12 kwa mwezi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...