Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akifurahia jambo na bi Mwaija Ngaga mara baada ya kufanikiwa kumaliza mgogoro wako
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye meza moja na walalamikiwa pamoja na walalamika wakati wa kutatua mgogoro
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutatua mgogoro


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi saba dhidi ya chuo kikuu cha Iringa uliodumu toka mwaka 1992

Akizungumza kwenye ofisi za mkuu wa chuo hicho,Kasesela alisema kuwa amefanikiwa kuutatua mgogoro huo kutokana na kuzikutanisha pande mbili ambazo zilikuwa zinagombana kuhusu ardhi ya chuo hicho ilipochukuliwa mwaka 1992.

“Huu mgogoro ni wa miaka mingi na mimi nimeukuta hivyo leo nimefanikiwa kuumaliza kwa njia ya busara kabisa kitu ambacho pale zilizokuwa zinalalamika zimefikia muafaka” alisema Kasesela

Aidha Kasesela alisema kuwa wamefanikiwa kumaliza mgogoro kwa kuwatafutia kila mmoja kiwanja kimoja ili kufidia maeneo ambayo serikaliilikipatia chuo kikuu cha Iringa.

“Nimewaagiza uongozi wa chuo kuwa ikifika siku ya jumatatu waje ofisini kwangu ili wawalipe nauli zao hawa wananchi kwa kuwa wanawajibu kwa mujibu wa makubaliano yetu ambayo tulikuwa tumefikia kwenye kikao hiki” alisema Kasesela

“Kwa leo nimefalijika kuona familia hii imeamua kumaliza mgogoro huu ambao ulikuwa hauna afya katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi hawa kwa kuwa walikuwa wanapoteza muda mwingi kupigania mgogoro huu” alisema Kasesela

Kwa upande wa waliokuwa wanalalamika wakiwakilishwa Mwaija Ngaga pamoja na Zuhura Balama walisema kuwa wamelidhishwa na maamuzi yaliyofikiwa na kumpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa kwa kumaliza mgogoro huo.

“Kwa kweli mkuu wa wilaya tunaomba ufikishe salamu zetu kwa Rais kwa kuchagua viongozi kama nyie wenye maono ya kushughulikia kero za wananchi maana la sivyo tulipanga kwenda Dodoma kumuona Rais” walisema wazee hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...