Na Woinde Shizza, Ngorongoro

Moja ya maeneo yaliyomo kwenye orodha ya maajabu saba ya dunia ni
Mamlaka ya Hifadhi ya Nogorogoro yenye vivutio vingi vya utalii
akiwemo faru mweusi.

Hifadhi hiyo ina mamlaka inayojitegemea kwa kuwa na majukumu tofauti
yanayolenga kuhifadhi viumbe hai na makazi endelevu kwa ajili ya
vilivyopo na vijavyo.

Lakini kwa upande mwingine, upekee wa Ngorongoro unatokana na jinsi
lilivyo eneo lenye hifadhi mseto ambapo kuna viumbe hai aina tatu
vikiishi kwa pamoja, yaani watu, mifugo na wanyamapori.

Hillary Mushi ni Naibu Kaimu Kamishna wa Uhifadhi katika Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro anaelezea mambo mbalimbali yahusianayo na
mnyama huyu aina ya Faru mweusi ,tabia zake ,huonekana wapi,sehemu
ambayo anaonekana ,dhamani yake pamoja na mambo mengine mengi endelea kufatilia ili umjue zaidi Mnyama huyu.

Faru ni nini?
Pamoja na kuwapo wanyamapori kwenye eneo hilo, Farumweusi aliye
miongoni mwa jamii hiyo ya wanyamapori wakubwa, anatokea katika
familia ya Rhino-cerotidae.Faru huyo anaakisi jina la kiingereza Rhinoceros ama faru na siokifaru kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya watu.

Mnyama huyo ni miongoni mwa wanyama pori watano wakubwa barani Africa,wakiwamo pia chui, simba, mbogo na tembo.Kuonekana
Kwa hapa nchini, Ngorongoro inatajwa kuwa sehemu nzuri ya kuwaona faru
wakiwa kwenye eneo la bonde maarufu kama crater.

Wanyama pori hao wamekuwa wakiongezeka kutokana na ulinzi uliowekwa naMamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, huku serikali ikijitahidi kuwalinda
wasipotezwe kwa njia ya ujangili.

Kutokana na umuhimu wao kwa nchi, serikali imewawekea ulinzi maalum
wa masaa 24 unaofanywa na askari wa wanyama pori.
Aina za faruMbali na faru mweusi, kuna ainatano za faru duniani, huku Africaikiwa na aina mbili yaani weupe na weusi. Aina nyingine tatu
zilizobaki zipo kusini mwa bara la Asia.

Kwa sehemu kubwa, faru mweupe na faru mweusi wanafanana na wote wanamaumbile yanayovutia kuwatazama. Pamoja kufanana huko, faru mweusi nimdogo kimaumbile kuliko faru mweupe, na wana mdomo uliochongoka kwaajili ya kukusanya majani kabla ya kula,faru mweusi ana mdomouliochongoka kuliko faru mweupe.

Wataalamu wa wanyamapori wanaeleza kwambakwa asili, faru haweza kuishiakifikisha kipindi cha miaka 35 - 50, lakini hali sivyo kwa faru
mweusi mwenye uwezo wa kuishi hadi kufikisha miaka zaidi ya 55.

Mfumo wa faru kuishi maisha ya kujitenga huku dume na jike wakikutana
katika msimu wa kujamiiana, tena kwa kutafutana kwa njia ya harufu
ambayo hutolewa na jike pale anapokuwa anamuhitaji dume.

Inapotokea hali hiyo, faru hubeba mimba kwa kipindi cha siku 475 au
miezi 16, japokua wakati mwingine hufikisha zaidi ya miezi 18. Kwa
kawaida faru huzaa ndama mmoja na mara chache anaweza kupata mapacha.

Ndama wa faru anapozaliwa, mwili wake huwa umefunikwa na manyoya ya
kahawia.Manyoya hayo humsaidia kumlinda asichomwe na jua wakati wa
mchana na kumkinga dhidi ya baridi wakati wa usiku.

Ndamadume wa faru anapofikisha umri wa miaka miwili na ndama jike
anapofikisha umri wa miaka minne huwatoroka wazazi wao na kwenda
kujitegemea. Kitendo hicho kinatoa fursa kwa faru jike kwenda kutafuta
dume na kubeba mimba nyingine.

Faru mweusi anafahamika zaidi kwa umbo lake kubwa na ni miongoni mwa
wanyama wanaokula nyasi, huku wakikaribia kuwa na uzito wa tani moja.

HimayaUwezo wa faru mweusi kuanzisha himaya inategemea na uimara na nguvu zafaru dume. Kama atakuwa dhaifu, atabaki kukimbizwa kila mahali na faruwanaomiliki eneo husika.

Faru dume huanza kupanda wakati akifikisha umri wa miaka saba wakati
jike anapandwa akiwa na umri wa miaka minne.Baada kitendo hicho,
wanyamapori hao huachana, na faru dume anaweza kupanda majike mengi
kadiri ya idadi yiliyopo.

Thamani ya faru mweusiThamani ya faru weusi ipo zaidi kwenye pembe zake zinazoelezwa kuwa naprotini, sawa na ile inayopatikana kwenye nywele na kucha.Pia Faru mweusi, kutokana na jinsi anavyovutia watalii wa ndani na
nje, anachangia kuingiza pato la taifa linalotokana na sekta ya
utalii.

Maadui wa faru mweusiKama walivyo wanyamapori wengi hasa waliopo kundi la kutoweka, farumweusi pia anakabiliwa na changamoto ya ujangili, na pia simbawanaowawinda watoto (ndama) wao kwa ajili ya kitoweo.

Hillary Mushi ni Naibu Kaimu Kamishna wa Uhifadhi katika Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro, anaendelea kusema katika kipindi cha miaka ya
1980, kulikuwa na tishio la kutoweka kwa faru mweusi lakini ulinzi
uliongezeka kiasi cha kuwafanya waendelee kuwepo.

Akasema kumekuwepo dhana hasi inayoenezwa na majangili wa
wanyamaporikwamba viungo vya faru hasa pembe vinahitajika sana katika
nchi za Asia kwa vile vinatumika kutengeneza dawa na mapambo, na hivyo
kulipiwa fedha nyingi kwa ununuzi wake.

Miongoni mwa hoja inayojengwa kuhusu viungo hivyo vya faru ni kwamba
zinatengeneza dawa zikiwemo za kuongeza nguvu za kiume.“Wanawaaminisha watu kuwa nguvu za kiume za faru zinazomfanya ampandejike kwa takribani dakika 40 zinazopatikana kwenye pembe zake, jamboambalo limethibitishwa na wataalamu kwamba si kweli,” anasema.

Ulinzi zaidiMamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro intambua umuhimu wa faru na hivyokujipanga kwa kuweka mikakati ya ulinzi dhidi ya wanyamapori haowaliopo kwenye hatari ya kutoweka.

Mkakati huo unahusisha hamasa na elimu kwa jamii inayoishi ndani na
maeneo ya kuzunguka eneo la mamlaka, ili washiriki kuwalinda
wanyamapori hao dhidi ya majangili.

Francis Ole Siapambuni ni mfugaji wa jamii ya Kimasai anaoishi ndani
ya Mamlaka a Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Alisema Hifadhi hiyo
inamazingira mazuri ya mapito ya wanyamapori na malisho ya mifugo pia
Hifadhi hiyo ina sehemu maalumu kwa ajili ya wanyama aina ya pofu na
nyani kuzalia pamoja na ndege aina tofauti,uku akibainisha wanyama
ambao wanapatikana Ndani ya mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni wengi
na wanavutia watalii haswa wanaotoka nchi za Mke.

"wageni wakija kuona faru hawa weusi wanaingiza kipato kwaiyo
tunafurahi maana tunanufaika sisi kutokana na mapato yanayotokana na
ugeni huu ,maana tunajengewa Shule hospital pamoja na zahanati kwaiyo
tunajivunia bonde letu la creater pamoja na wanyama
tulionao"Siapambuni.

MUONGOZA WATALII ALONGA.

Akiongelea Mnyama huyu muongoza utalii aliejitambulisha kwa jina la
Bakari Uledi alisema kuwa watalii wengi wanapenda kuwaona faru weusi
kwani wanavutia sana na kunabaadhi ya watalii haswa wazee ambao
wamewaleta katika hifadhi hii na hawakubahatika kuwaona faru weusi
wanasijitika sana na wanaondoka kwa uzuni kwani Wengi wao unakuta
wamekuja kuona wanyama wengine lakini wanatamani sana kumuona mnyama
huyu faru.

Aidha alibainisha kuwa kunawageni wengine wamekuwa wanakuja na pindi
wakimaliza kutembelea hifadhi na unakuta hawajabahatika kumuona Faru
mweusi wamekuwa wakiaidi kurudi kurudi kwa ajili tu Kuwaona

Mafanikio Kamishna wa Uhifadhi wa mamlaka hiyo, Freddy Manongi, amesema kunamafanikio katika kupambana na ujangili kwani katika kipindi cha miakaminne iliyopita, hakuna tukio la tembo wala faru aliyeuawa na
majangili.

Amesema wanajivunia rekodi hiyo kwani katika miaka minne ya uongozi wa
Rais John Magufuli,uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori huo umekuwa wenye
manufaa kwa nchi.

“Hakunamzoga wa faru au tembo ambao umeokotwa kwenye eneo la mamlakaau hata kuripotiwa kwenye hifadhi nyingine nchini kwamba kuna mnyamakauawa na majangili,” anasema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...