Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini hapa leo, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa 2019 yanayo tarajiwa kuanza kufanyika mkoani Singida kuanzia kesho. 
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na Waandishi wa habari ukiendelea.


Na Dotto Mwaibale, Singida 

MAADHIMISHO ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Singida ambapo Tanzania itaungana na nchi wanachama wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) katika kusherehekea siku hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi alisema mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kuwa yatazinduliwa kesho katika Uwanja wa Bombadia.

" Ndugu Wananchi napenda kuwafahamisha kuwa mkoa wetu wa Singida umepewa heshima na Taifa kuwa mwenyeji wa Siku ya Chakula Duniani.Maadhimisho haya yatazinduliwa kesho Oktoba 10, 2019 natoa wito kwa wananchi wa Singida na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Bombadia ambako maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia kesho na kufikia kilele chake Oktoba 16, 2019.

Dkt. Nchimbi alisema kaulimbiu ya maadhimisho hayo inasema “Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa” na kuwa kauli mbiu hiyo inalenga kuhamasisha jamii na wadau wote wa sekta kilimo kuchangia katika kuhakikisha nchi na dunia inakuwa na chakula cha kutosha wakati wote.

Alisema Takwimu za Wizara ya Kilimo zinaonyesha hali ya upatikanaji chakula mwaka 2019/2020 ni nzuri, kwani nchi, ina chakula cha kutosha. Kiwango cha utoshelevu wa chakula ni asilimia 119. Uzalishaji wa mazao ya chakula ulifikia tani 16,408,309 ukilinganisha na mahitaji ambayo ni tani 13,842,536. Kati ya hizo Tani 9,007,909 ni mazao ya nafaka na tani 7,400,400 ni mazao yasiyo nafaka.Tunawapongeza watanzania kwa kutekeleza kauli mbiu hii kwa vitendo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...