Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya kamati inayoshughulikia kuhamasisha na kuondoa mimea vamizi mkoa wa Arusha.
Na.Veronica
Ignatus,Arusha
Serikali
mkoani Arusha imeitaka kamati inayoshughulikia kuhamasisha, na kuondoa mimea
vamizi ,kutoa elimu kwa kushirikiana na wataalamu kwa taasisi
mbalimbali za serikali, ikiwemo mifugo,Kilimo,Mazingira na wizara ya Afya, mashuleni na maeneo mbalimbali ya jamii juu ya mimea vamizi wa gugu karoti.
Kauli hiyo
imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega, kwa niaba ya
mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ,kwenye siku ya maadhimisho ya siku ya gugu
karoti na visumbufu vingine vya mazao mkoani Arusha ,iliyofanyika wilayani
Arumeru ,katika Taasisi ya Utafiti wa viwatilifu kwa ukanda wa kitropiki
(TPRI)Mkoani hapa.
Kwitega amesema
kuwa bila ushirikiano wa pamoja kati ya wataalamu, wadau wa maendeleo ,kazi
hiyo haitakuwa na maana wala mafanikio ,hivyo kila mmoja analojukumu la
kuhakikisha anafanyakazi kwa nafasi yake, ili elimu na uelewa iwafikie jamii kwa
ujumla katika mapambano hayo.
Ametoa wito
kwa Waandishi wa habari ambao ni wadau muhimu na jeshi la mianvuli, kutumia
vyema kalamu zao kuhabarisha jamii juu ya gugu hilo vamizi ,kwa kutoa elimu kwa umma
juu ya madhara na namana ya kuliangamiza gugu hilo.
Ndelekwa
Kaaya ni mwenyekiti wa Kamati uhamasishaji wa kudhibiti gugu hilo, amesema
kuwa dhumuni la siku hiyo ni kuwahamasisha na kutoa Elimu ya uelewa kwa wadau wa kilimo,mifugo,mazingira,afya ya
binadamu,viongozi wa dini,viongozi wa kimila taasisi za Elimu ,makundi maalum
watafiti ,wanasayansi ,wafanyabiashara viongozi wa siasa wafahamu kuhusu madhara
na udhibiti wa Gugu karoti na visumbufu vamizi katika mkoa wa Arusha, na mikoa
mingine ambapo kuna visumbufu vamizi.
Amesema
katika siku hiyo mada mbalimbali zinazohusiana na ueneaji usambaaji na mbinu,njia
za kuzuia na kudhibiti visumbufu vamizi zitatolewa na wataalam mbalimbali toka
taasisi za serikali na sekta binafsi ili kujenga uelewa kwa jamii ya
watanzania.
Amesema kuwa
jitihada zilizofanywa na kamati katika harakati za kudhibiti gugu hilo ni
pamoja na kushirikiana na taasisi binafsi ,zimeweza kufanya utambuzi wa
visumbufu vamizi ,na kuainisha maeneo yalipovamia.
Ameinisha changamoto zinayoikabili kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yake ni pamoja
na ukosefu wa rasilimali fedha, kwaajili ya kuwezesha uhamasishaji wa kuzuia na
kudhibiti visumbufu vamizi, ikiwemo kuwafikia wadau wengi katika maeneo
yaliyovamiwa mkoani Arusha .
Aidha ukosefu wa vifaa vitendea kazi ,vifaa kinga vinavyotakiwa kutumika
katika zoezi la ung’oaji wa visumbufu vamizi haswa katika maeneo mbalimbali
katika barabara za jiji la Arusha, ambapo ushirikiano mdogo kutoka kwa wadau
wenyewe katika maeneo yaliyovamiwa na visumbufu vamizi likiwemo gugu karoti .
Ramadhani
Kilewa ni Mtafiti kitengo cha kidhibiti visumbufu vya mimea kutoka (TPRI) amesema
kuwa aina hiyo ya visumbufu vya wadudu na wanyama ni tatizo katika mikoa yote
nchini Tanzania,ambapo maeneo mengi yaliyovamiwa ni mashamba ya mazao ,malisho ya
wanyama,Hifadhi za taifa ya Arusha ,Ziwa manyara , Serengeti na Ngorongoro,maeneo
ya makazi ya watu ,maeneo ya kutunza na kusambaza nishati ya umeme ,mabwawa ya
maji kwaajili ya matumizi ya binadamu na
wanyama.
Kilewa ameyataja madhara yatokanayo na gugu hilo kuwa ni pamoja na magonjwa ya aleji ya
ngozi kwa binadamu na wanyama,kifua kinachobana (pumu)kwa binadamu,umasikini katika ngazi ya familia, kata ,wilaya na
mkoa.(pumu)kwa binadamu.
Kiuchumi
gugu hilo linasababisha kupungua kwa mavuno ya mazao ya chakula na
biashara,Athari katika biashara ya utalii na wanyama kushindwa kupita kwenye
baadhi ya mimea vamizi,maziwa ya wanayama wanaofugwa kuwa na uchungu kwasababu
ya sumu iliyomo katika mimea vamizi,upungufu wa malishio ya wanyama pamoja
madahara kwa afya ya udongo na uoto wa asili na uharibifu wa mazingira
Aidha asili ya gugu hilo kwamba ni Amerika ya Kusini,A.kati na A.Kaskazini
maeneo ya Mexico, hapa nchini Tanzania liliingia mwaka 2010 limetokea nchini Ethiopia,ambapo mmea mmoja huweza
kutoa mbegu 15,000 ,25,000-100,000 na zinauwezo wa kuzaa kila baada ya miezi 4,mmea mmoja unaweza kutoa miche kwa mara tatu,unauwezo wa kukaa
ardhini kwa miaka kumi.
"Zinaene kwa
njia ya upepo,utengenezaji wa barabara,upepo binadamu wenyewe,asaia
,Afrika,visiwa ,Austaralia Afrika ya kusini,nchi zote za afrika ya nmashariki
kwa afrika zaidi ya 13,kwa Tanzania taarifa iliyopo ni mikoa mitano,inaathiri
uoto wa asili,inazuia
mbegu za mazao zisiote ,inasaidia uzaliaji wa wadudu,vimelea vya magonjwa
kwenda kwenye mazao mengine,inzi weupe.Alisema Kilewa.
MWISHO
H
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...