Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni akimlisha keki mmoja wa watoto wa darasa la awali katika Shule ya Mikocheni A ikiwa ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwapongeza mmoja wa watoto aliyesoma vizuri risala kwa niaba ya watoto wenzake
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni akikagua darasa kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali linalokarabatiwa kwa ufadhili wake.
Meya Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akipata viburudisho na wanafunzi.
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda akiwapongeza mmoja wa watoto aliyesoma vizuri risala kwa niaba ya watoto wenzake.

******************************

MEYA Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amewaomba wadau mbalimbali nchini kujitokeza kwa namna mbalimbali kuchangia elimu ili kuleta ustawi bora katika jamii .

Ametoa rai hiyo jana wakati alipokuwa akikabidhi moja ya darasa katika shule ya Msingi Mikocheni ‘A’ alilolikarabati kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali hatua iliyoendana na hafla fupi na watoto hao ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa.

Mbali na ukarabati huo Meya huyo mstaafu pia alikabidhi viti na meza kwa ajili ya wanafunzi hao wa darasa la awali ili kuwaondolea changamoto ya ukaaji pindi wanapokuwa darasani.

Mwenda alisema kama jamii itajenga utamaduni wa kuzikumbuka shule walizosoma na kwenda kutoa misaada inayohitajika katika shule hizo kwa kiasi kikubwa watakuwa wametoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya shule hizo na sekta nzima ya elimu nchini.

“Serikali inafanya mambo mengi sana katika elimu lakini nasi kama wananchi hatuna budi kujitokeza na kuiunga mkono ili iweze kutimiza azma yake kikamilifu kwa kuchangia japo kidogo kwa kile tunachojaaliwa kuwa nacho” alisema Mwenda

Awali Mwenda alipata fursa ya kutembelea mazingira ya shule hiyo na kujionea hali ya uchakavu mbalimbali wa majengo hatua iliyotokana na kujengwa miaka mingi huku uongozi wa shule hiyo ukimuomba kuwasaidia ukarabati wa ofisi ya walimu.

Walisema kutokana na uchakavu wa majengo ya shule hiyo wamelazimika kutumia moja ya darasa kuwa ofisi yao licha ya kukosa sifa zinazotakiwa na kwamba wanafanya hivyo kutokana na uwepo wa changamoto ya majengo mahali hapo

Aidha Mwenda alilikubali ombi hilo na kuhahidi kulifanyia kazi ili kuwaondolea walimu hao adha wanayoipata wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...