Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Oktoba 8, 2019 wakati akitangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba 2019 ambao umeshuka hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano na Kaimu mkurugenzi waTakwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja leo Oktoba 8, 2019 wakati akitangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2019 ambao umeshuka hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.
(Picha zote na MAELEZO)


Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi septemba, 2019 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watukutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja wakati akitangaza mfumuko wa bei leo Jijini Dodoma.

“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019 ikilinganishwa na bei za kipindi cha Septemba,2018”. Alisisitiza Bi. Minja.

Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.

Aliongeza kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Akizungumzia nchi za Afrika Mashariki Bi. Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei nchini Kenya kwa mwezi Septemba umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka 5.00 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Kwa upande wa nchi ya Uganda, mfumuko wa Bei kwa mwaka unaoishia mweziSeptemba 2019 umepungua hadi asilimia 1.9 kutoka asilimia 2.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...