Na Judith Mhina-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametoa funzo kubwa kwa Watanzania kuwa tunahitaji kuwatengeneza watumishi aina ya Rais Magufuli ili Tanzania iweze kusonga mbele.

Sio mara moja wala mbili Rais Magufuli amekuwa akijiuliza maswali kadhaa kutokana na utendaji anaokutana nao katika ziara zake mikoani, na hatma ya Tanzania huko tunakoelekea. Hii ina maana kubwa kwetu na ni vema kupata majibu hayo kwa mstakabali wa Taifa letu.

Rais Magufuli amekuwa akijiuliza maswali kadhaa ambayo mimi na wewe kutoa majibu kwa haraka itakuwa ni uongo. Bali  kama Watanzania tunawajibu wa kumuahidi Rais  kuwa kutokana na utendaji wake uliotukuka, tumeona kinachojiri kwa sasa hapa Tanzania kwa kweli maendeleo makubwa yaliyopatikana  na yanayoendelea  kupatikana ni wajibu kuwatengeneza Magufuli wengi kwa mstakabali wa Taifa letu.

Baadhi ya maswali hayo ambayo kila uchweo, katika ziara zake mikoani au wakati za kuapisha viongozi mbalimbali  Rais Magufuli anajiuliza na anasema “Je nikiondoka leo  Bwawa la Umeme la Nyerere litajengwa? Nikiondoka leo reli ya kisasa (SGR) itajengwa Je Nikiondoka leo ndege zitanunuliwa? Hapa ndipo napata nguvu ya kufanya kazi.”  

Rais Magufuli nguvu anayoipata kwa ajili ya kutimiza azma yake katika kuleta maendeleo  Tanzania, ndipo anapochochea azma ya vijana na watanzania wenye uchungu na nchi hii kufikiri na kutafakari kwa nini na wao wasiwe watendaji wazuri kama Rais Magufuli?.

Maneno ya uchungu anayojiuliza Rais Magufuli yawe  chachu kwa vijana  kutafakari  na kuahidi kila mmoja nitaifanyia nini Tanzania. Kila kijana wa Tanzania ajiwekee mikakati yake binafsi  kwa kuangalia mifano hai ya utendaji wa Rais Magufuli na kuahidi kufanya vema  akiwa katika sekta binafsi hapo alipo au sekta ya Umma.

Kitabu cha Uongozi na Hatma ya Taifa la Tanzania cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kimeeleza wazi aina ya kiongozi anayepashwa kuiongoza Tanzania. Aidha miko na taratibu za uongozi ni lazima zifuatwe ili kuhakikisha ustawi wa Taifa lolote lile duniani.

Kwanza Rushwa ni Adui wa Haki suintatoa wala kupokea rushwa tuwatengeneza vijana ambao wana nia ya dhati na dhamira zao zinatuambia kwake hakika rushwa ni adui wahaki. Sifa hii Rais Magufuli ameidhibitisha kuwa ameipiga vita rushwa kwa nguvu zote, hususan kupambana na watu wenye fedha au kipato cha juu, Hakika kwa hili hongera na pongezi unastahili.

Vita dhidi ya madawa ya lulevya, ambayo ni vita kali sana duniani kwa kuwa wahusika wana uwezo wa kutoa rushwa ya kiasi chochote kilecha fedha,  kwa serikali na watendaji wake. Lakini Rais Magufuli amefanikiwa kuimarisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa- TAKUKURU.

Pia, kuanzisha Tume ya Kuratibu Uthibiti wa Dawa za Kulevya –Drug Control Commission of Tanzania, ikiwa na kujitolea kwa vijana shupavu kama na wa mfano kama, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam Mhe. Paul Makonda, hiki ni kithibitisho vijana wakuendeleza unayoaanza wapo.     
Baba wa Taifa amesema Rais tumtakaye ni yule ambaye anaweza kutetea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuhakikisha unadumu milele.  Kwani ndio kielelezo cha Umoja wetu, Amani Upendo na Mshikamano, ambao ndio dira yetu  na tunu ya Taifa letu.

Rais Magufuli ni kiongozi ambaye ameonesha kielelezo hicho kwa uwazi na kuahidi kuudumisha Muungano huo, kwa nguvu zake zote akili na maarifa aliyojaliwa na Mwenyezi Mungu. Nina hakika wapo vijana ambao wanautetea Muungano huu na kuenzi kwa nguvu akili maarifa na moyo wao wote.

Mfano wa mambo yanayoimarisha Muungano ni uwepo wa Wizara za Muungano ambao unafahamika, lakini wapo mawaziri kutoka upande wa pili wa Muungano ambao wanashika nyadhifa ambazo sio wizara za Muungano, ikiwemo masuala ya msamaha wa deni la Tanesco kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.  
Kiongozi tumtakaye ni lazima aone nyufa za Muungano na awe na uwezo wa kuziba nyufa hizo  kabla hazijaleta madhara. Rais Magufuli amelidhibitisha hilo na nachukua kila hatua ya kuhakikisha Muungano wetu unakuwa imara zaidi kuliko wakati wowote .

Baba wa Taifa amesema Tanzania inataka Rais ambaye atakuwa Mtumishi na sio Mtawala, kiongozi anayeumizwa na shida na mahangaiko  ya Watanzania. Rais Magufuli amethibitisha hili kwa kusema sipo radhi kuongoza Watanzania wanaotoa machozi.  Rais anahangaika usiku na mchana kuhakikisha anatatua shida na mahangaiko mbalimbali ya Watanzania.

Tumeshuhudia Rais akichukizwa na ulanguzi wa korosho za wakulima na kuingilia kati ili wasidhulumiwe jasho lao, lakini pia kujua haki zao kama wakulima. Amechukizwa na ufujaji wa fedha za Umma kwenye sherehe ambazo hazina tija  na kuzipeleka kufanya usafi wa mazingira na kupambana na ugonjwa wa kipindupindu na kununua dawa.

Serikali ya Awamu ya Tano inakusanya kodi kwa kila mtu bila ubaguzi, kwa mara ya kwanza katika historia  ya nchi imevunja rekodi ya kukusanya  fedha za Tanzania Trilioni 1.8 kwa mwezi  Agosti 2019. Nyerere alisema katika moja ya hotuba zake serikali corrupt haikusanyi kodi, inabaki kukimbizana na wafanya biashara wadogo wadogo.  

Rais Magufuli ameumwa na mahangaiko ya wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga ) amekuja na mfumo madhubuti ya kuwafanyia wafanye biashara zao kwa uhakika zaidi bila kubughudhiwa. Kuanzishwa kwa vitambulisho maalum vya Rais ndio kielelezo cha kuonyesha ni jinsi gani anaumizwa na mahangaiko ya watanzania.

Rais tumtakaye ni yule anayeweza kuwa mbunifu kutokana na rasilimali tulizonazo na kuhakikisha Taifa linajitegemea ili kuleta heshima. Rais Magufuli amelitekeleza kwa kutumia fedha za ndani katika kujiletea maendeleo, sasa nchi inaheshimika  ukikataa na fedha zako haijalishi nchi inasonga mbele. Vijana wanaona Rais anavyofanya wanajifunza wanakuelewa kwa kuwa wazalendo wapo.

Kuanzishwa kwa sera ya Elimu bure Tanzania kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne kila mwezi serikali inatoa jumla ya Bilioni 23. 5 kwa ajili ya Elimu bure shule za sekondari na za Msingi Tanzania Bara.

Kwa sasa kuna vijana wengi sana ambao wapo shule  na hawahangaiki tena na kukimbizana na Walimu, Wazazi wafadhili na wengineo katika kutafuta fedha za ada. Matokeo yake hata watoto wa maskini kwa sasa wapo shule.  Ndio hao hao  watakaokuja kuchukua nafasi za uongozi katika nchi hii na hakika tutambue vijana wanaona anachofanya Rais Magufuli.

Tumeshuhudia miaka mingi inapita migogoro ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji, Wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi ikiwemo hifadhi za Taifa. Rais Magufuli hili limemuuma Sana na kuhakikisha jumla ya vijiji 920 kati ya 975 nchini vilivyopo maeneo ya hifadhi vimetambuliwa rasmi.  Yote haya kwa masilahi ya watanzania wanyonge vijana wanaona nina hakika watafata nyayo zako.

 Aidha, Tanzania imefuta maeneo ya akiba 12 yenye ekari 707, 659, 95 na misitu 7 yenye ekari 46,715. Pia serikali imeamua kumega eneo la hifadhi 14 ili kuwapa wananchi maeneo ya kuishi kuzalisha kilimo na ufugaji ambapo katika uamuzi huo vijiji 60 vinavyonufaika ni  vya Mkoa wa Katavi.
Kiongozi bora ni yule anaweza kutoa suluhisho la kudumu kwa watu wanaohusika badala ya kubaki na ngonjera za utafiti unafanywa, tupeni muda serikali inalifanyia kazi,  nimeagiza viongozi watatoa mustakabali wa tatizo hilo. Utasikia mchakato unaendelea miaka nenda miaka rudi.  

Kitabu cha Uongozi wa Tanzania na Hatma yake cha Baba wa Taifa Nyerere kinasema Rais tumtakaye ni yule anayeguswa na matatizo ya majirani zake Rais Magufuli ameonyesha Mfano wa kuhakikisha majirani zake waliopata dhoruba ya kimbunga cha Kenneth kilichotokea mapema mwezi April 2019 na kuadhiri Malawi, Msumbiji, Zimbabwe, na kuhakikisha Tanzania inatoa msaada wa tani za mahuindi kadhaa kwa Malawi Zimbabwe na Msumbiji.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika –SADC kwa sasa imepamba moto na nchi ya Tanzania ndio Mwenyekiti, ambapo imeonyesha dira kwa kuzindua Kituo cha Huduma za Pamoja za Mpakani, Nakonde One Stop Post ili kuongeza mtengamano wa Jumuiya hiyo katika masuala mbalimbali ya Bishara, Mawasiliano, Uchukuzi na mengineyo.   

Rais wa Tanzania awe ni yule anayetaka kuwaletea maendeleo watanzania sio kujiletea maendeleo yeye mwenyewe, familia yake na marafiki zake. Rais magufuli ametia fora katika eneo hilo barabara  nyingi zimejengwa nchi nzima kwa kiwango cha lami, barabara hizi ni kichocheo kikubwa cha uchumi, Rais Magufuli  vijana wanaona na kuona ni kuamini.

Vituo vya Afya 320 Zahanati na Hospitali za Wilaya kadhaa za Rufaa Mkoa zimejengwa na kuimarishwa, Bajeti ya dawa imeongezwa na dawa zinapatikana hospitali zote za serikali kutoka Bilioni 32  mpaka Bilioni 352. Vyumba vya madarasa vingi vimejengwa ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Awamu ya Tano.

Rais tumtakaye ni yule anayehimiza Umoja Mshikamano Upendo kwa Watanzania na ndio maana Tanzania na ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki imetengemaa, uanzishwaji wa Umoja wa forodha katika mipaka ya Tanzania na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
Aidha, Ushirikiano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika –SADC ni kielelezo kingine ambacho kinaonyesha Tanzania imeadhimia kuhakikisha dhamira ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ya Umoja wa Afrika inatimizwa.

Rais tumtakaye ni yule asiye na ubaguzi wa dini, rangi sura eneo atokalo mtu kabila au vinginevyo. Watanzania wote ni sawa na Afrika ni moja Rais Magufuli anasema “Naomba mniombee nisibadilike niwatumikie Watanzania kwa moyo wangu wote akili na maarifa, naomba nisibadilike nisiwabague Watanzania kwa kabila zao, dini zao, rangi zao maeneo wanayotoka naomba mungu anisaidie”

Rais Magufuli amesema “Siwezi kuendesha nchi ambayo watu wake wanatoa machozi”  Viongozi wetu wametimiza wajibu wao, uamuzi ni wa Watanzania kuamua kutumikia nchi yao kwa nidhamu na heshima, upendo na amani kila utendalo liwe kwa masilahi ya nchi na sio vinginevyo. Rais magufuli matendo yako yatatengeneza MAGUFULI  WENGI WAJAO MUNGU IBARIKI TANZANIA.      

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...