MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amewaongoza baadhi ya watendaji wa benki hiyo kugawa chai kwa wateja wao.
Akizungumza akiwa kwenye tawi la Kariakoo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Nsekela alisema ni wiki muhimu kwa wateja wa CRDB.
Alisema ni wiki ya viongozi wa benki hiyo kutoka matawi yote kuwafuata na kuwahudumia wateja kwa upendo chini ya kaulimbiu ya 'Ulipo tupo kukupa Magic'.
"Hii ni wiki ya huduma kwa wateja duniani kaulimbiu ya dunia ni 'The magic of service' na sisi benki yetu tunashiriki kwa kuwahudumia wateja wetu.
"Tunawaambia ulipo tupo kukupa Magic. Tumeandaa vitu vingi vizuri naamini wateja wetu watafurahia," alisema Nsekela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akifungua Shampeni kuashiria kuanza kwa wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa sehemu mbalimbali duniani, katika hafla iliyofanyika kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Karikoo jijini Dar es salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimiminia Shampeni mmoja wa wateja wa Benki hiyo, waliofika kupata huduma kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Karikoo jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...