
Na HAJI MANARA
Inawezekana utawala wao hauna mbwembwe kama za Haji Manara, na umekosa umaarufu kwa baadhi ya Mashabiki wa soka nchini, lakini nathubutu kuandika utawala huu wa sasa wa Shirikisho la Soka nchini TFF ndio utawala unaoonyesha mafanikio makubwa ya maendeleo ya uwanjani Kwenye mchezo huu kuliko utawala wowote huko nyuma.
Hebu tuanzie miaka ya sitini baada ya uhuru hadi sasa na tukiyatembelea maneno ya Chairman Mao ya "No research No Data No right to Speak"
Nani anaweza kulinganisha mafanikio ya utawala huu wa sasa wa TFF na zilizopita?
Ngoja nikueleze machache kisha unijibu swali langu pendwa,
Kwa mara ya kwanza baada ya Uhuru,Tanzania imeandaa Mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF ( Afcon Under 17 ) Baada ya miaka thelathini na tisa Tanzania imeshiriki fainali za Mataifa ya Afrika,
Baada ya miaka kumi Tanzania inarejea tena Kwenye Mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ( CHAN).
Hapa sote tunajua yaani kufuzu kwetu kwa AFCON na CHAN ni ndani ya mwaka mmoja huu wa 2019,
haipo TFF yoyote huko nyuma na hata tukisema FAT iliyowahi kuiwezesha nchi hii kubwa kufuzu katika mwaka mmoja Mashindano hayo yote kwa wakati mmoja ( FACT ISIYOGUSIKA)
Kufuzu tena kwa timu Kwenye Afcon under 17
Kuchukua ubingwa wa CECAFA Kwa timu yetu ya under 20,
Kuchukua ubingwa kule Kampala
Timu yetu ya taifa ya vijana kushinda Cecafa kule Burundi,
Kushinda kikombe tena kwa timu ya vijana kule Botswana na Rwanda
Kushinda kwa timu za taifa za Wanawake kubwa na ile ya vijana Mashindano mbali mbali ya COSAFA na CECAFA kule Afrika kusini na Rwanda, lakini kuiwezesha Taifa Stars kwende Kwenye makundi ya kufuzu kwa kombe la dunia la mwaka 2022 kule Qatar.
Niwaarifu hayo yote yamefanyika katika kipindi cha miaka miwili tu, tena mengi kati ya hayo ni mwaka huu wa 2019.
Sasa nani anaweza kunyoosha kidole juu akanitajia TFF au hata FAT ambayo ktk kipindi cha mwaka mmoja au miwili wamefanya haya?
Ndio maana nilimsafiria Chairman Mao ambapo mm nnaeandika makala hii ni muumini wa falsafa zake nilizozikalia darasani.
Haiyumkiniki kuupinga ukweli uliowazi na tutafanya dhambi kuu isiyohitaji usamehevu wowote ule.
Tanzania kwa miaka mingi tumekuwa Pombe ya ngomani, kila aliyepo anajichotea tu, al-muhimu uwe na chombo cha kunywa, iwe kikombe, glasi, kopo na hata kifuu, twende!!
Ila sasa heshma yetu inaanza kurejea taratibu na sasa tukiwa uwanjani, wenzetu Afrika wanasema Yes, nchi inacheza!!
Hapo sijaongelea mafanikio makubwa ya Simba msimu huu ya kuwa klabu ya kwanza tokea uhuru kufuzu kwa hatua ya Robo fainali kutoka ktk makundi ( Groups Stage) ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Nawezaje kuacha kuitaja TFF hii ni mafanikio ya Simba msimu uliopita ilhali wao ndio wenye mpira wao nchini?
Sisemi kwamba TFF hii haikosei na haijakosea,. mm msingi wa makala yangu ni mafanikio ya uwanjani ambayo ndio Watanzania wanayataka.
Narudia tena na tena, MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.
Sote tunajua wanazo changamoto nyingi na mapungufu yao kama Binadaam lakini katika hili la matokeo ya uwanjani wao ni namba wani kulinganisha na Nyimati za tawala zingine za TFF/FAT Huko nyuma.
Siku nyingine nikijaaliwa ntaandika changamoto na kasoro zao uongozi huu madhubuti ulio chini ya Rais Chief Wallace Karia na mtendaji mkuu Mido kisheti Wilfred Kidao.
Najua katika eneo la ukosoaji mm ni mzuri zaidi ya kusifia, hvyo nna imani ntawafurahisha sana Wakosoaji wa Tawala hii bora kabisa ya soka nchini kuwahi kutokea.
Nice weekend.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...