Eliud Kipchoge amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili

Raia huyo wa Kenya alikimbia muda wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindani la Ineos Challenge mjini Vienna nchini Austria siku ya Jumamosi.

Haitatambulika kuwa rekodi mpya ya dunia katika mbio hizo kwa kuwa halikuwa shindano la kila mtu mbali na kwamba alitumia kundi la wanariadha wa kusukuma kasi waliokuwa wakishirikiana naye na kutoka.

Bingwa huyo wa Olimpiki alikuwa ameikosa rekodi hiyo na sekunde 25 katika jaribio lake la hapo awali 2017.

Alipogundua kwamba alikuwa anakaribia kuweka historia , wanariadha waliokuwa wakidhibiti kasi ya mbio hizo walirudi nyuma na kumwacha bingwa huyo kutimka hadi katika utepe huku akishangiliwa na mashabiki wengi mji mkuu wa Austria.

Bingwa huyo mara nne wa London Marathon alimkumbatia mkewe, akachukua bendera ya Kenya na kukumbatiwa na wanaraidha waliokuwa wakimsaidia kuweka muda huo bora wakiwemo mabingwa katika mbio ndefu duniani.

Katika mitandao ya kijamii walimwengu walimpongeza kila sekunde aliyokimbia hadi kumaliza mbi hizo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...