Na Mwandishi wetu - Dodoma

Wizara ya Nishati (Tanzania) na Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Oktoba 17, 2019 walikutana katika ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma na kujadili Mkakati wa kufikisha gesi asilia katika mikoa mbalimbali nchini.

Kikao hicho, kilichoongozwa na Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi, kilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara, Haji Janabi na maafisa kutoka wizarani na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC.)

Katika kikao hicho, JICA waliwasilisha rasimu ya Mkakati tajwa waliouandaa kwa kushirikiana na watalaamu wa Wizara na TPDC.

Mkakati huo umeainisha mahitaji ya nishati kwa mikoa mbalimbali nchini na kupendekeza namna bora ya kufikisha gesi katika mikoa hiyo kulingana na mahitaji.

Aidha, mkakati huo umejumuisha uchambuzi wa kiuchumi kwa kila njia pendekezwa ili kuona ni ipi itakuwa na manufaa zaidi. Njia zilizopendekezwa ni kupeleka gesi kwa njia ya mabomba, gesi iliyogeuzwa kimiminika au gesi iliyogandamizwa.

Wizara kupitia TPDC inatekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya kusmbaza gesi asilia na kuunga wateja katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Mtwara kwa kuanzia.

Kukamilika kwa Mkakati wa kufikisha gesi katika mikoa mingine na kuanza kwa utekelezaji wake, kutawezesha wananchi wengi zaidi katika mikoa mbalimbali nchini kutumia gesi asilia ambayo ni nafuu na rafiki kwa mazingira ikilinganishwa na vyanzo vingine vya nishati.

Ujumbe wa JICA uliongozwa na Kenekiyo Kenekiyo, Mshauri katika Taasisi ya Masuala ya Nishati Japani (IEEJ)
Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi (katikati), akiongoza kikao baina ya wataalamu wa Wizara ya Nishati na Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), kilichojadili Mkakati wa kufikisha gesi asilia katika mikoa mbalimbali nchini. Kikao kilifanyika Oktoba 17, 2019 Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...