Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kushoto) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo Kanali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Erasmus Bwegoge ikiwa ni udhamini wa NMB kwa timu ya JWTZ inayotarajia kushiriki michezo ya majeshi ulimwenguni. Kulia ni Meja wa JWTZ, Wilfred Abedinego akishuhudia.
Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ikiwa ni sehemu ya udhamini wa NMB kwa timu ya jeshi inayotarajia kushiriki michezo ya majeshi ulimwenguni, vifaa hivyo vinathamani ya shilingi milioni 18. Kulia ni Kanali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Erasmus Bwegoge.

Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kushoto) akimkabidhi jezi Kanali wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Erasmus Bwegoge ikiwa ni sehemu ya udhamini wa NMB kwa timu ya JWTZ inayotarajia kushiriki michezo ya majeshi ulimwenguni. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Wateja Binafsi, Ally Ngingite pamoja na Meja wa JWTZ, Wilfred Abedinego (kulia) wakishuhudia.
 
Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana vifaa hivyo vya michezo

********************************

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ikiwa ni udhamini wao katika michezo mitatu, yaani mchezo wa ngumi, mieleka pamoja na mchezo wa riadha.

Udhamini huo wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 18, umekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Biashara ndogo na za Kati, Filbert Mponzi kwa viongozi wa JWTZ.

Aidha akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Bw. Mponzi alisema Vifaa hivyo vya Michezo vilivyotolewa na NMB ni sehemu ya udhamini wa Benki ya NMB kwa Michezo ya ngumi, mieleka pamoja na riadha.

Aliongeza kuwa, Benki ya NMB inaushirikiano mkubwa na wa muda mrefu ambao umekuwa na faida kwa pande zote huku ukiendelea kuimarika siku hadi siku.

“…Kwa niaba ya NMB tunaomba mtuwakilishe vema na tutafurahi zaidi mkirudi hapa na medali za dhahabu, tutakuwa na furaha zaidi kwani si tu mmeshinda bali benki yetu itakuwa imeshiriki kufanikisha ushindi huo,” alisema Bw. Mponzi akikabidhi msaada huo.

Alibainisha kuwa NMB imekuwa ikishirikiana na JWTZ kudhamini michezo mbalimbali, jambo ambalo linaendelea kuboresha mahusiano mazuri kati ya pande zote.

Michezo ya Majeshi Duniani, World Military Games inayoshirikisha majeshi mbalimbali ulimwenguni, inatarajia kufanyika nchini China katika Jiji la Wuhan hivi karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...