Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Frank Mwaisumbe
amewapongeza Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) kwa
kubadili mfumo wa utendeji kazi wake na kuondoa urasimu wa utendaji
kazi, kwani urasimu hupelekea shughuli nyingi kukwama kupelekea
wawekezaji wengi kukimbia nchini kutokana na vikwazo.
Mwaisumbe
aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, amesema hayo
jiji Arusha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakaguzi
wa Usalama na Afya kutoka OSHA na WCF, amesema juhudi za kupunguza tozo
kumeisaidia OSHA kuweza kuwafikia Wawekezaji wengi zaidi na hivyo suala
la Usalama na Afya Mahali Pa kazi kuanza kutekelezwa na kuzingatiwa na
Waajiri wengi hapa nchi.
“Nimefarajika kusikia kwamba,
mmeendelea kuboresha huduma zenu, hilo ni jambo jema. Waajiri wengi
nchini hawatapendi kuona urasimu, wengi wao wawekezaji wakiona kuna
urasimu huondoka na kutafuta sehemu zingine ili waweze kuwekeza” amesema
Mhe. Mwaisumbe .
Mhe. Mwaisumbe amesema juhudi hizi
ambazo zimefanywa na OSHA zimekuja kipindi kizuri hasa kipindi hiki nchi
inapotekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Miradi ya Umeme,
Ujenzi wa Barabara, Madaraja, ambapo watu wengi huajiri.
Naye
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda amesema mafunzo hayo
yameandaliwa kwa lengo la kuwaongezea uwezo watumishi wa Umma kwa lengo
la kutoa huduma bora katika maeneo yao ya kazi. Amesema Wakala
unaendelea kuboresha huduma zake, hivyo mafunzo hayo yataongeza ufanisi
kwa wakaguzi wawapo kazini.
Khadija amesema yakuwa wakati
nchi inaendelea kupiga hatua mbalimbali za kiuchumi na mabadiliko
mbalimbali ya Kiteknolojia duniani, mafunzo kama haya yatakuwa muafaka,
yataenda sambasamba na kuwafunza wakaguzi mbinu mpya za kukabiliana na
mabadiliko hayo pamoja na changamoto.
“Wenzetu hawa huko
kwao masuala ya usalama na Afya yanazingatiwa na yanapewa kipaumbele,
sasa ujuzi ambao wakaguzi wataupata kutoka kwa wataalamu hawa
yatasaidida kuboresha utendaji kazi wetu, na mbinu mpya za kuweza
kufanikisha zoezi zima la kufanya kaguzi za usalama na Afya,” amesema Bi
Mwenda.
Naye, Mjumbe wa Shirika la Workplace Health without
Borders (WHWB), Aristides Medard kutoka Tanzania ambao ni Waratibu wa
Mafunzo hayo kwa kushirikiana na OSHA kwa upande wa Tanzania amesema
lengo kubwa la taasisi hiyo ni kuhakikisha linatoa mafunzo yanayolenga
kuondoa changamoto mbalimbali za usalama na Afya Mahali pa kazi duniani
ambazo hujitokeza.
Mafunzo haya ya wiki
moja yameandaliwa na OSHA kwa lengo la kuwajengea uwezo wa wakaguzi wa
OSHA pamoja na WCF, namna bora ya kufanya kaguzi, na yanaendeshwa na
wakufunzi kutoka CANADA,MAREKANI na UBELGIJI kutoka shirika la kimataifa
la Workplace health without Border (WHWB).
Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda akizungumza na Wakaguzi wa Usalama na Afya kutoka OSHA na WCF wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakaguzi hao jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Frank Mwaisumbe akizungumza na Wakaguzi kutoka OSHA wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wakaguzi hao ambapo amewapongeza Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...