Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete amewahamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kuandika vitabu pamoja na kujenga tabia ya kusoma vitabu kwani kwa sasa changamoto iliyopo watu wengi hawasomi vitabu ukilinganisha na miaka ya zamani.

Kikwete ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kuomba kutoa salamu na mtunzi wa kitabu kinachozungumzia kwa kina uhusiani wa nchi za Tanzania na China ambacho kimeandikwa na Joseph Kahama ambacho kinafahamika kwa jina la The Challenge to China-Tanzania Relationship to Enhance Cooperation and Matual Benefits.

Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bara Philip Manglla.Mbali na Mangulla viongozi wengine wa ngazi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda wameshuhudia uzinduzi wa kitabu hicho.

Wakati Rais Kikwete anazungumza beads ya kuombwa kusalimia , ametumia nafasi hiyo kupongeza Kahama kwa uamuzi wa kuandika kitabu hicho ambao ametumia nafasi hiyo kuwahimiza Watanzania kujenga tabia ya kuandika vitabu.

"Binafsi nimeanza kuandika kitabu ambacho kwa sasa kina kurasa 270 na bado naendelea maana kila ninapoandika mambo mengi yanakuja.Sina hakika kama Desemba mwaka huu nitakuwa nimekimaliza kukiandika.Najua muda inayotumika kuandaa kitabu,hivyo nampongeza Hoseph Kamaha kwa kutengua muda wa kuandaa kitabu hiki ambacho naomba Watanzania wakipate na kukisoma.

"Hata hivyo naomba nieleze tu siku hizi tunauogonjwa mkubwa wa kutopenda kusoma vitabu au kuandika.Watu hawasomi kabisa vitabu,wamekuwa wagumu kweli.

"Nakumbuka wakati nasoma sekondari nilikuwa na utamaduni wa kusoma sana vitabu na ninaendelea na utamaduni huo,miaka ya nyuma Watanzania walipenda sana kusoma vitabu,"amesema Kikwete na hivyo ameshauri watu kupenda kusoma vitabu na kuongeza "Siku hizi watu muda mwingi wameshika Laptop labda ndio humo humo wanasema vitabu".

Kuhusu kitabu hicho amesema hajapata kukiona kabla ya kuzinduliwa,hivyo kwa kuwa kimezinduliwa atatakikisha anakisoma kwani kwa maelezo ya waliokisoma kitabu hicho wameeleza kwa kina  mambo ya msingi yaliyoandikwa na Mwandishi wa kitabu hicho ambacho kinazungumzia historia ya Tanzania na China.

"Mwandishi Mwandishi ambacho akizungumza ameweka na takwimu,hii inathibitisha namna ambavyo amefanya tafiti za kutosha na kujiridhisha kwa kile ambacho amekutumia kukiandika.

Kwa upande wake Hoseph Kahama Kahama akizungumzia kitabu hicho ameeleza kwa kina sababu za kuandika kitabu hicho ambacho kinazungumzia urafiki baina ya Jamhuri ya Watu wa China  na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 55 na umekuwa wa kipekee na imara katika nyanja mbalimbali.
Rais mstaafu Jakaya Jakaya Kikwete akizungumza kuhusu umuhimu wa Watanzania kujenga utamaduni wa kusoma vitabu.Rais ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kitabu cha The Challenge to China-Tanzania Relationship to Enhance and Mutual Benefits kilichoandikwa na Joseph Kahama ambaye ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kukuza Uhusiano China na Tanzania.
Balozi wa China China nchini Tanzania Wang Ke akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu ch The Challenge to China-Tanzania Relationship to Enhance Cooperation and Mutual Benefits kilichoandikwa na Joseph Kahama.
 Rais mstaafu Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda wakati anaingia ukumbuni kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa kitabu hicho.

 Baadhi ya waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...