Na, Editha Edward -Tabora

Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amefanya Ziara yake mkoani Tabora na kukagua maendeleo ya viwanda vilivyopo mjini hapo ambapo ameonesha Kutoridhishwa na utendaji kazi pamoja na uzalishaji wa kiwanda cha nyuzi TABOTEX

Waziri bashungwa amefika katika kiwanda cha nyuzi ambapo amejionea uzalishaji Katika kiwanda hicho ambacho kilibinafisishwa kwa muwekezaji Rajan tangu mwaka 2004 kutoka kwenye Mikono ya Serikali kikiwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi zaidi ya Mia mbili ambapo uzalishaji wa nyuzi ulikuwa ni wastani wa tani elfu tatu na Mia sita kwa mwaka 

Akiwa katika kiwanda hicho waziri bashungwa ametembelea na kushuhudia kushuka kwa uzalishaji pia na kuwa na idadi ndogo ya wafanyakazi katika kiwanda hicho

Naye mbunge wa Tabora mjini Emmanuel Mwakasaka ameonesha Kutoridhishwa juu ya kiwanda hicho kwamba hakioneshi matumaini kwani tangu mwaka jana hadi leo hakijabadilika kitu chochote kwenye kuongeza wafanyakazi na kuongeza uzalishaji wa bidhaa

"Nimekuja mara ya mwisho hapa ila cha kushangaza hadi sasa sijaona mabadiliko wa sipidi ambayo inayotakiwa sasa hivi kwa viwanda sijaona pamoja na sasa tunaenda na kwa teknolojia lakini kiwanda kama kingekuwa kinaendeshwa vizuri kisingekuwa na wafanyakazi wachache kama hawa waliopo''Amesema Mwakasaka

Katika hatua nyingine waziri bashungwa amebainisha msimamo wa Serikali ya Awamu wa Tano ambayo dhamira yake ni kukuza uchumi wa Taifa kupitia viwanda vya hapa nchini 

"Wamiliki wa viwanda mnaniangusha sana serikali, mnatakiwa mboreshe utendaji wenu wa kazi panueni wigo wa masoko na muongeze uzalishaji wa bidhaa zenu"Amesema Bashungwa

Aidha katika Ziara yake waziri bashungwa pia ametembelea kiwanda cha mazao ya misitu Tabora pamoja na kiwanda cha maziwa ambapo akiwa Katika kiwanda cha maziwa ameagiza shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO kuwaunganisha wawekezaji wadogo na kampuni kubwa ili waweze kuimarika zaidi.
 Pichani ni Waziri wa Viwanda na biashara  Innocent Bashungwa (Katikati)  akiwa katika kiwanda cha nyuzi  TABOTEX,  Tabora.
Pichani ni Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa akipewa maelekezo na meneja wa kiwanda cha maziwa cha Tabora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...