Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

OFISA Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (44) na mwenzake mmoja, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin. 

Mbali na Mwamgabe, mshtakiwa mwingine aliyefikishwa mahakamani hapo ni Abrahamani Msimu (54) dereva na mkazi wa Yombo jijini Dar es Salaam. 

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Aldolf Lema amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando kuwa Agosti 25 mwaka jana katika eneo la Posta jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 124.55.

Washtakiwa hao pia wanadaiwa, Agosti 25, 2018 katika eneo la Posta, walisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa gramu 1.55.

Hata hivyo, washtakiwa hao walikana kutenda makosa hayo na wako huru kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama iliwataka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili mmoja kutoka ofisi za umma watakaosaini bondi ya Sh. Milioni tano kila mmoja. 

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Washtakiwa hao wametimiza masharti ya dhamana na kesi itatajwa tena Oktoba 16 mwaka huu.
 OFISA Usalama wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (44) na mwenzake mmoja, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...