Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV

Maadhimisho ya Siku ya unywajj kahawa Duniani, yamefanyika Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera, huku takwimu zikionesha kuwa Asilimia 7. pekee ya Watanzania wote, ndio watumiaji wa kinywaji hicho licha ya faida kedekede zinazopatikana kwa Mtumiaji wa  Kahawa.

Mgeni Rasmi Sherehe hizo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu  pamoja na mambo mengine, katika hotuba yake ametumia
 mwanya huo kumpongeza Mshindi na Mkulima Bora wa zao la Kahawa Tanzania kwa msimu wa Kahawa 2018 - 2019, Bwn. Albert Katagila kwa kutunukiwa Tuzo hiyo, ambayo aliipatiwa na Bodi ya Kahawa Tanzania wakati wa Sherehe za Nane nane Mwaka huu Mkoani Simiyu, na ndio sababu ya Sherehe hizo kufanyika Kyerwa.

Mhe. Mwaimu amesema kuwa Serikali ipo bega kwa bega na Wakulima, na changamoto ndogo ndogo zitashughulikiwa, huku msisitizo zaidi ukiwa kwa Wananchi na Wakulima wenyewe, kunywa kahawa kwa Wingi, na kuomba wawekezaji kuongeza Viwanda Mkoani Kagera ili kahawa hiyo iweze kuuzwa kwa bei nzuri katika soko, kwani kwa kufanya hivyo itaongeza Chachu ya Kufikia adhma ya Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli ya Tanzania ya Viwanda, huku kahawa hiyo ikimnufaisha Kiuchumi Mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Aidha Mkulima bora wa zao la kahawa ambaye pia ni Mkurugenzi wa JJAD KAGERA FARMS Ndg. Albert Katagila amesema kuwa, mafanikio ya kufikia heshima aliyopewa ya kutunukiwa Tuzo hiyo ni kutokana na juhudi za makusudi ambazo amefafanua kuwa, ni pamoja na Usafi wa mashamba ya wakulima ambayo husababisha kukinga zao la kahawa dhidi ya magonjwa na wadudu, pia Ubora wa kutotumia dawa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika ili kahawa iweze kushindanishwa na Kahawa nyingine katika Soko la Dunia , na mwisho ni namna ya Uvunaji, uanikaji na uhifadhi wa kisasa wa kahawa hiyo,  kwa kufuata maelekezo kupitia maafisa ugani, ambao wanaweza kuinusuru sekta ya Kilimo.

Sanjari na hayo Wakulima waliohudhuria sherehe hizo wameishukuru Serikali kwa namna inavyozidi kuwatengenezea mazingira bora, na rafiki kwao Kwa kuwawezesha kupata pesa zao kwa haraka zaidi, huku wakulima hao wakihoji wapi maganda yanapelekwa baada ya kahawa yao kukobolewa, huku wakitaka rasilimali hiyo ikibidi arudishiwe mkulima kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.
Pichani Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu akikabidhi cheti kama Tuzo ya Ushindi kwa Mkulima Bora wa Kahawa Bwn. Katagila wakati wa Sherehe za Kuadhimisha Siku ya Unywaji Kahawa Duniani, Oktoba Mosi ambapo Kitaifa zimeadhimishwa Mkoani Kagera.
 Pichani ni moja ya aina ya Kahawa ya Robusta iliyomenywa inayodaiwa kuwa na gharama katika soko hasa Nchini Ujerumani kama Ilivyokutwa na kamera yetu.
 Pichani Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu akionja Kahawa wakati wa Sherehe za Kuadhimisha Siku ya Unywaji Kahawa Duniani, Oktoba Mosi ambapo Kitaifa zimeadhimishwa Mkoani Kagera.
 Pichani ni sehemu ya shamba la Mkulima Bwn. Albert Katagila Mkulima bora wa msimu wa zao la kahawa Baada ya Michuzi kutembelea shamba hilo.
 Pichani Ni Mkuu wa Wilaya Kyerwa Rashid Mwaimu akiwa ameketi na Mkulima Bora wa Kahawa Tanzania Bwn. Albert Katagila wakionja kahawa wakati wa Sherehe za Siku ya Unywaji Kahawa.
 Pichani Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu akihutubia Wakulima na wananchi  wakati wa Sherehe za Kuadhimisha Siku ya Unywaji Kahawa Duniani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...