Na Said Mwishehe, Michuzi Blog

KAMPUNI ya Miranda Investment kwa kushirikiana na Serengeti Media Centre, Chuo cha Utalii Serengereti na Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu ya Wazanaki imeandaa tamasha kubwa la Kumbukumbu ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambalo linatajia kufanyika kuanzia Oktoba 8 hadi Oktoba 14 Butiama Musoma mkoani Mara ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu wa kwanza wa Rais Joseph Warioba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi utamaduni wa Wazanaki Mashaka Mgeta amesema kuna umuhimu mkubwa wa kufanyika kwa tamasha hilo na kwamba ni miaka 20 tangu Mwalimu Julius Nyerere, hivyo wao kampuni hiyo wameona kuna umuhimu wa kufanya tamasha hilo ambalo pamoja na mambo mengine litawaleta Watanzania pamoja.

Amesema tamasha hilo ambalo limebeba kauli mbiu ya Uadilifu na Uchapakazi ni dira ya kuufikia uchumi wa viwanda na kwamba Mwalimu Nyerere alipambana sana katika ukombozi wa Taifa la Tanzania. Mgeta ameongeza wakati taifa linamkumbuka Mwalimu Nyerere, kupitia tamasha hilo wananchi kutoka Mkoa wa Mara na mikoa jirani watapata burudani za kila aina kupitia michezo mbalimbali ambayo imeandaliwa kwa mwaka huu.

Kwa upande wake Mtaribu wa Tamasha hilo Kulwa Karedia amesisitiza kama Watanzania wanavyotambua kila ifikapo Oktoba 14 ya kila mwaka nchi yetu huadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa ,Hayati Mwalimu Julius Nyerere na kwa mwaka huu maadhimisho hayo ni ya 20.

Amesema kuwa maadhimisho haya huambatana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali, vikundi na watu binafsi, lengo kubwa ni kumkumbuka mwasisi wa taifa letu kutokana na kujitoa kwa kila namna dhidi ya utawala dhalimu wa kikoloni na hatimaye kuleta uhuru ambao tunajivunia kwa kuupata bila kumwaga damu.

"Tunatambua mwalimu Nyerere alilifanyia taifa hili mambo ambayo hayawezi kufutika kamwe machoni mwa Watanzania. Kutokana na msingi huo, tuliopo tunapaswa kumuenzi kwa kuyaendeleza yote mazuri aliyoyafanya. Kwa kutambua uzito wa hili, Miranda Investment, Serengeti Media, Chuo cha Utalii Serengeti na Kituo cha Kuendeleza Utamaduni wa Wazanaki, tumeandaa tamasha na kongamano la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambalo litaanza kuunguruma Oktoba 8- 14 kijijini Butiama mkoani Mara,"amesema Karedia.

Pamoja na Serikali kuwa na siku ya kitaifa ambayo inaadhimishwa mwaka huu mkoani Lindi kwa shughuli mbalimbali, zikiwamo sherehe za kuzima Mwenge wa Uhuru ambao Mwalimu Nyerere aliuasisi, tumeona ni jambo jema na la msingi tuungane na wakazi wa kijiji cha Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla kukumbuka siku hiyo muhimu kwa kufanya tamasha la burudani kwa michezo mbalimbali.

Pamoja na mambo mengine amesema kubwa ni kuwapo kwa mashindano ya riadha yaliyopewa jina la Mwalimu Nyerere Historical Marathon yakiwakilisha wanariadha kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara na nje ya mkoa huo."Tamasha hili tutashirikisha pia wananchi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mara, Tarime, Bunda, Musoma, Butiama na Serengeti na mikoa ya jirani kama Mwanza, Simiyu na Arusha,"amesema.

Kuhusu matukio yatakayofanyika katika tamasha hilo Karedia amesema ni riadha, Mbio za Kilomita 10, Mbio za Kilomita Tano kwa vijana kati ya miaka 13 - 18.Pia kutakuwa na mbio za kilomita mbili na nusu , mbio za kujifurahisha
Karedia amesema mbio zote zitaanzia Uwanja wa Mwenge Butiama kupitia Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kuelekea Barabara ya Kiabakari ambayo Mwalimu Nyerere aliitumia wakati wa kuunga mkono matembezi ya Azimio la Arusha mwaka 1967.Pia kutakuwa na mbio za baiskeli, bonanza la mpira wa miguu na kuongeza kuwa timu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mara zimealikwa kushiriki, wakiwamo mabingwa watetezi Butiama Stars 

Pia kutakuwa na mpira wa pete ambapo Karedia amesema kwa mwaka huu wameboresha zaidi mashindano hayo kwa kuongeza mchezo wa mpira wa pete, maana wanaamini mwalimu alikuwa mpenzi wa kila kundi. Tunagetemea timu kutoka wilaya zote zitafika Butiama.

Amefafanua kuwa mchezo wa bao nao utakuwapo kwenye tamasha hilo hasa kwa kuzingatia Baba wa Taifa, alikuwa mchezaji hodari wa mchezo huu, kutokana na hali hiyo, tumealika timu zaidi ya sita kutoka Sengereti, Musoma, Tarime na Butiama. Hapa tunagemewa kivumbi kutimka kwa sababu kuna wazee waliobebea, wataonyeshana umwaba hapa.

Wakati huo huo kutakuwa na ngoma na kwaya ambapo vikundi vya ngoma za asili na kwaya vitashiriki. "Tunagetegea kuwa na wageni mbalimbali wa kitaifa na kitamaifa. Nasema hivi kwa sababu tumefanya mawasiliano na balozi kadhaa kama ule wa Marekani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda, Msumbiji,Afrika Kusini na China,"amesema Karedia .

Wakati huo huo amesema washiriki zaidi ya 1,000 kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Mara na maeneo jirani wanatarajiwa kushiriki tamasha hili Tunamshukuru Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Mara, Profesa Sospter Muhongo kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha mno wana Mara kujitokeza.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu mstaafu na Makamu wa Kwanza wa Rais Jaji Joseph Warioba. Pia wanatarajia uwapo wa wakuu wa wilaya, wabunge na viongozi wengine kutoka mikoa ya jirani.

Karedia ametoa mwito kwa kuwaomba wakazi wa Mkoa wa Mara na mikoa ya jirani wajitokeze kwa wingi kushiriki tamasha hili ili kumuenzi Mwalimu Nyerere wa vitendo, tukiongozwa nakauli mbiu ya mwaka huu katika tamasha hilo inasema hivi: Uadilifu na uchapakazi ni dira ya kufikia Tanzania ya Viwanda

 Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi  Kumbukumbu ya Utamaduni wa Zanaki Mashaka Mgeta akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  kuhusu tamasha la kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere linalotarajia kufanyika Butiama wilayani Musoma mkoani Mara .Kulia ni Mratibu wa tamasha hilo Kulwa Karedia.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu ya utamaduni wa Wazaki Mashaka Mgeta(kushoto) akiwa na Mratibu wa tamasha la kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha hilo linalotarajia kufanyika Butiama mkoani Mara
 Mratibu wa Tamasha la Kumbukumbu ya miaka ya 20 ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Julius Nyerere, Kulwa Karedia(kulia) akizungumzia ratiba ya  shughuli zitazofanyika wakati wa tamasha hilo linalotarajia kuanza Oktoba 8 hadi Oktoba 14 mwaka huu Butiama mkoani Mara .Kushoto Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhifadhi Kumbukumbu ya utamaduni wa Wazanaki Mashaka Mgeta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...