Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Tandahimba Khadija Mwinuka akifafanua jambo
shule ya msingi Amani iliyopo Tandahimba mjini
Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Tandahimba Khadija Mwinuka amesema anajipanga kuondoa tatizo la watoto kutojua kusoma na kuandika wanapomaliza elimu ya msingi.
Amesema hayo wakati akizindua mashindano ya Wilaya ya Kusoma,Kuandika,Kuhesabu na Kuchora ambayo yamefanyika katika shule ya msingi Amani iliyopo Tandahimba mjini
" Wanafunzi ambao wamemaliza mwaka huu 34 walikuwa hawawezi Kusoma wala kuandika hii ni changamoto,lakini lengo letu ni kutokuwa na wanafunzi wa namna hii ndani ya Wilaya yetu,"amesemaMwinuka
Amesema wanafunzi 54 wa darasa la Kwanza na la pili wanashindana na wanatarajia kupata wanafunzi 8 ambao watakwenda kwenye mashindano ya Mkoa na baadaye Kitaifa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...