Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Utegi Enterprises (T)LMT Otieno Igogo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu udhamini wa michuano ya mchezo wa mpira wa miguu kuelekea katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere Octobar 14 mwaka huu.Kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo Shaban Mparure.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
TIMU 14 kutoka Kata ya Msigani Kinondoni jijini Dar es Salaam zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kuwania kombe la kumbukumbu ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo yaliyoanza Septemba 14 mwaka huu kwa kuwa na timu 48 na kwamba timu ambazo zimeingia hatua ya nusu fainali ambayo itaanza kutumia vumbi kuanzia Jumamosi ya wiki ijayo.
Katika kuhakikisha ushindani unakuwa mkubwa kwenye michuano hiyo Zawadi za vikombe na medani zitatolewa katika timu ambazo zitashika nafasi ya kwanza na ya pili ambapo timu hizo zitafanyika katika makundi matatu na kila kundi linatimu nne.
Akizungumza zaidi leo Oktoba 4 ,mwaka huu jijini Dar es Salaam mmoja wa waandaaji wa mashindano hayo Shaban Mparure amesema katika kuhakikisha michuano inakuwa na ushindani walishirikisha timu hizo 48 na timu 12 kati ya hizo ndio zimefanikiwa kuingia hatua hiyo ya nusu fainali.
Amesema kuwa mashindano hayo yamedhaminiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya UTEGI Techical Enterprises (T) LTD Otieno Igogo ambaye ndio ametoa vikombe na zawadi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini Mashindano hayo ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Mparure amesema fainali za mashindano hayo zinatarajia kufanyika katika Uwanja wa wa Uhuru jijini Dar es Salam kuazia Oktoba nane hadi Oktoba tisa na kwamba kadri siku zinavyozidi kwenda watatoa ratiba kamili ya fainali hizo.
Kuhusu zawadi za washindi amesema mshindi wa kwanza atapata Kombe kubwa na mpira mmoja na zawadi wa mshindi wa pili itakuwa mpira mmoja.Pia kutakuwa na zawadi ya mchezaji bora.
Mparure amesema lengo kubwa la kufanya mashindano hayo ni mwendelezo wa kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikuwa mpenda michezo na mzalendo wa nchi yake na Afrika kwa ujumla.
Awali akizungumzia udhamini wake Mwenyekiti huyo wa Kampuni ya Utegi interprises (T) LTD Otieno Igogo amesema kuwa Mwalimu alikuwa zawadi ya pekee kwa ajili ya kuikomboa Afrika na mzalendo wa nchi yake na kwamba alihamasisha watu kuwa katika misingi hiyo pia aliweza kuunganisha nchi katika misingi ya umoja wa kitaifa.
Igogo amesema kwamba Nyerere alijenga misingi mizuri ya kikatiba na uhuru wa habari pia aliruhusu uwepo wa mfumo wa vyama vingi na msingi mzuri wa kielimu.
Igogo amesema wao kama Kampuni wamejikita kwenye biashara ya forodha na zaidi ya miaka 35 ana endelea na kazi hiyo kuazia Mwaka 1984 .na amekuwa alifanya kwa nidhamu kubwa mno ikiwamo kulipa stahiki zote za Serikali.
Ameongeza kuwa yote ambayo anaya fanya ni katika kuendelea kumuenzi Mwalimu Nyerere na hasa kwa kutambua Oktoba 14 mwaka huu Watanzania tuna adhimisha miaka 20 ya kukumbuka ya kifo chake.
Amesema ni matumaini yake kupitia mashindano hayo ya kumuenzi Mwalimu Nyerere vijana watapa nafasi ya kutambua mchango wa Mwalimu katika kuhakikisha nchi yetu inakuwa na umoja,upendo na mshikamano na leo hii hakuna anayezingumzia ukabila wala udini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...