MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu  Askari  Polisi watano na Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kulipa faini ya Shilingi milioni 7.6 ama kutumikia kifungo cha mwaka miaka saba gerezani baada ya kukiri kosa la kuiba mafuta ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Washitakiwa hao, Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47) wa JWTZ, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson  na PC Hamza ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi walifutiwa mashtaka ya utakatishaji fedha na kupanga genge la uhalifu na kubaki na mashtaka ya wizi.

Kabla ya kufutiwa mashtaka yao, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Renatus Mkude alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo kuwa, wameingia makubaliano na washitakiwa hao kumaliza shauri hilo hivyo, aliomba makubaliano hayo yawe sehemu ya shauri hilo.

Hakimu Mwaikambo alisema ni lazima mahakama ijiridhishe kama ni kweli washitakiwa waliweka makubaliano hayo kwa hiari bila kulazimishwa ndipo wakasema kuwa, waliandika makubaliano hayo wenyewe.

Akisoma adhabu, Hakimu Mwaikambo amesema amezingatia kwamba washitakiwa ni wakosaji wa kwanza na kuwa amezingatia msamaha uliotolewa na rais wa washitakiwa kukiri makosa yao na kupunguziwa kiwango cha makosa yao.

"Kila mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 au kifungo cha miaka saba jela, pia mtatakiwa kulipa thamani yote mliyosababisha hasara kwa ATCL yaani Sh 4,647,760. Pia magaloni yote ya mafuta yanataifishwa na kuwa mali ya serikali," amesema Hakimu Vick.

Mapema kabla ya kusomwa hukumu hiyo,  Wakili Mkude aliieleza mahakama kuwa hawana taarifa ya nyuma ya washitakiwa hao na kwamba shauri hilo limeingia utaratibu wa makubaliano hivyo, suala la adhabu tunaiachia mahakama lakini pia tunaomba warudishe hasara waliyosababisha na kutaifisha madumu 109 ya mafuta ya ndege.

Kwa upande wake, wakili wa utetezi, Nestory Wandiba amedai washitakiwa wameokoa muda wa mahakama kwa kukubali kosa na kwamba kosa linalowakabili adhabu yake ni kifungo cha miaka saba au faini.

Katika kesi hiyo inadaiwa Julai 30, mwaka huu huko katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washitakiwa  waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik) yenye thamani ya Sh  4,647,760 mali ya ATCL.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...