Tangu mwaka 2015 Tanzania ilianza mchakato kwa kufanikisha mapinduzi ya viwanda. Kama ilivyotanabaishwa katika Mpango wa Maendeleo, nchi inalenga kufikia uchumi wa viwanda, na kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Kwa sasa serikali imefanya kazi kubwa ya kuimarisha uchumi wa kitaifa kwa kuwa na aina mbalimbali za viwanda, ikiwemo viwanda vya vyakula, madini, na utalii. Hili limechagizwa na muunganiko wa programu za uwekezaji zilizoanzishwa na serikali na kupata ufadhili kutoka sekta binafsi.

Moja ya kiwanda kikubwa ambaho kimekuwa kikichangia kufikia mpango huo ni sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi ambayo imekuwa na matokeo chanya katika maisha ya maelfu ya Watanzania.

Sekta hiyo imezalisha kwa kiwango kikubwa fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na ajira za moja kwa moja 3,000. Pia watu wengine milioni 1.5 wameajiriwa katika ajira zisizo za moja kwa moja kama vile watoa huduma kwenye vibanda.

Pia, upanuzi wa upatikanaji wa huduma za intaneti umeboresha upatikanaji wa huduma mbalimba kupitia simu kama vile huduma za kifedha. Huduma hizi zimeweza kuleta mfumo wa fedha ambao ni jumuishi kwa watu wote, ukiwezesha ufanyaji wa miamala kwa haraka na usalama zaidi, ukopaji, huduma za bima, kwa watu wote wa mijini na vijijini ambako hakujawahi kuwa na tawi la benki.

Sekta ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania inafanya vizuri, lakini bado ni muhimu kuendelea kuiimarisha na kuiboresha ili kuhakikisha inaendeleo kuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu zaidi.
Kuna hofu kuwa sekta hiyo inazidiwa uwezo na watoa huduma, jambo ambalo linahatarisha uwezo wao wa kuwekeza katika mambo mbalimbali ikiwemo ubunifu zaidi.

Katika hili, ni muhimu sana hatua ikachukuliwa kuweza kuimarisha hali ya soko.
Kuna haja ya msingi ya kuimarisha soko hilo kwani sio kwamba tu itasaidia kampuni hizo kuweza kuhakikisha zinaendelea kupata faida, lakini itazisaidia kampuni hizo kuweza kuwekeza zaidi katika miundombinu ya kidojitali.

Hivyo ni muhimu hatua hii ikachukuliwa kwa haraka katika kutengeneza sekta ya mawasiliano ambayo itaendelea kutoa huduma zenye ubunifu, na fursa za kiuchumi kwa Watanzania wote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...