Ukarabati wa Meli ya Mv.Victoria
na Mv Butiama katika Ziwa Victoria unaendelea kwa kufunga vifaa vipya na
Vyakisasa,Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwaka 2020.
Hayo yamesemwa na makandarasi anayefanya
ukarabati wa meli hizo,na kusema kuwa kwasasa wanaendelea na kazi ya kufunga
genereta mpya na kupaka rangi.
Taarifa Zaidi.
Ukarabati unaofanywa na kampuni
ya KTMI ya Korea Kusini kwa
kushirikiana Kampuni ya Songoro Marine
ya Tanzania unaendelea kwa kufunga vifaa vipya na vya kisasa ili meli hizo
ziweze kutoa huduma ya usafiri katika Ziwa Victoria..
Mkurugenzi anayesimamia
Miundombinu ya Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Sekta
ya Uchukuzi Mhandisi Thomasi Ngulika amesema kuwa ukarabati wa meli hizo
umefikia asilimia Hamsini na kazi hiyo ni yamiezi kumi na Mbili..
Nae Meneja Mradi wa kampuni ya
KTMI kutoka Korea Kusini Chang Hwan Lee amesema kuwa mradi huo utakamilika mapema
mwezi wa tatu mwaka 2020.
Baadhi ya vijana wanofanyakazi
katika meli hiyo akiwemo kijana Raymond Msuya ambaye anafanya kazi katika ukarabati wa meli ya Mv Victoria,wameiomba Serikali kuwapatia Ajira ya kudumu kwani wamepata
elimu ya kukarabati meli kutoka kwa wakorea ambao wanafanya nao kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...