Picha ya pamoja ya viongozi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)  na wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA)  baada ya kikao chao cha mashauriano kilichofanyika makao makuu ya BAKITA Kijitonyama, jijini Dar es salaam. 

Kutoka kulia waliosimama mbele ni Bi Mwanahija  Ali Juma (Katibu Mtendaji - BAKIZA), Dkt.Muhammed Seif Khatib( Mwenyekiti - BAKIZA), Dkt. Selemani Sewangi (Katibu Mtendaji- BAKITA) na Dkt. Method Samwel (Mwenyekiti - BAKITA) na wajumbe wengine.

Mkutano huo ulijadili mambo kadhaa ya mashirikiano ambapo ilisisitizwa kwamba mabaraza hayo mawili yafanye kazi kwa karibu ili kusadia Watanzania kutumia kiswahili kwa ufasaha na usahihi. 

Pia ulikubaliana kwamba wajumbe kutoka pande zote za Muungano wawe wajumbe wa Mabaraza yote mawili ili kuwepo na kiungo thabiti wakati  maneno mapya ya fani na kitaaluma( istilahi) yanapoandaliwa kwa ajili ya matumizi na kwamba ni vyema Mabaraza yote yashirikishwe kwa karibu na kukubaliana kwa maelewano.
Vile vile ilikubaliwa uandaliwe mkutano wa vyama vya Kiswahili  vya Tanzania kwa ajili ya kukiimarisha Kiswahili na kuleta utangamano wa wadau wa lugha hii adhimu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...