Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAZIRI wa Kilimo Japheth Hasunga amesema bei elekezi ya mbolea ya kupandia na kukuzia kwa msimu wa mwaka 2019/2020  imeshatolewa ambapo imeanza kutumika kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na hiyo ni katika kuhakikisha kunakuwa na utoshelevu wa chakula nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Hasunga amesema kuwa mbolea zote zinatakiwa kuuzwa kwa bei iliyopangwa na Serikali na si vinginevyo na mbolea aina nyingine zitapangiwa bei na wafanyabiashara kwa kuangalia mahitaji na hali ya soko ilivyo.

Aidha amesema baada ya kuanza kwa mfumo wa kuagiza mbolea kwa pamoja bei imeshuka kwa asilimia kati ya sita hadi 17 kwa kuangalia umbali uliopo (Mkoa ambapo mbolea inakwenda.)

Kuhusu gharama za usafirishaji wa mbolea Waziri Hasunga amesema kuwa;
"Tukumbuke kuwa kabla ya mfumo wa uagizaji wa pamoja haujaanza ilikua inafikia sh. 23,000 na sasa imepungua hadi kufika sh. 3500, hivyo ina manufaa na kwa sasa tumekuja na mifuko ya kilo tano, 10 na 25  ili wakulima wanunue kwa wanachohitaji," ameeleza.

Kuhusu bei ya mbolea katika msimu huu Hasunga amesema kuwa asilimia 90 ya mbolea inayotumika nchini imeagizwa kutoka nje ukitoa kiwanda pekee cha mbolea cha Minjingu kilichopo mkoani Manyara.

" Asilimia 90 ya mbolea tunayotumia nchini inayoagizwa kutoka nje hivyo wadau na watanzania wenye uwezo wajitokeze kuwekeza kwenye sekta ya mbolea ili gharama za mbolea zizidi kushuka zaidi," amesema.

Amesema kuwa bei iliyopangwa ni ya juu zaidi hivyo wanunuzi wanunue kwa kuzingatia bei hiyo bila kuvuka;

"Mbolea ya kukuzia (UREA) imepungua kutoka sh.57,482 hadi kufikia shi. 53,997 kwa mfuko wa kilo hamsini ambapo kuna punguzo la sh. 3485 sawa na asilimia sita," amesema.

Amesema kuwa mbolea ya kukuzia katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa mfuko wa kilo hamsini bei imeshuka kutoka sh. 48,500 hadi kufikia sh.45,280 Manyara ikishuka kutoka sh.58,339 hadi kufikia sh. 54, 830 huku Mkoa wa Iringa bei ikishuka kufikia sh. 53,934 kutoka 56,443.

Pia Mkoa wa Geita bei ya mfuko wa kilo hamsini imeshuka kutoka sh. 60,124 hadi 56,683,  Arusha bei ikishuka kutoka sh. 57,236 hadi 53,722, Songwe bei ikiwa ni shilingi 55,851 kutoka 59,360, Shinyanga bei ikiwa ni sh. 55,903 kutoka 58,996 na Rukwa bei ikiwa ni sh. 58,378 kutoka 61,102.

Amesema bei hizo zimeshuka kwa mifuko ya kilo zote huku bei ya rejareja ya mbolea hiyo ya kukuzia kwa mikoa ya Mashariki, Kati, Kusini na Kaskazini ikiwa ni kati ya sh. 45,800 hadi 47,100 na kwa Mikoa ya Magharibi, Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini bei ni kati ya sh. 52,400 hadi 59, 700.

Waziri Hasunga ametumia nafasi hiyo kuzionya Kampuni zinazouza mbolea feki na kutorosha mbolea kabla ya kuanza kutumika nchini kuacha mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kunyang'anywa leseni zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...