Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Simiyu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Baadhi ya Watumishi wa Umma kutoka Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mataka (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipotembelea ofisini kwake kabla ya kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika katika Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Katibu Msaidizi Ajira na Nidhamu, Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Celina Maongezi akiwasilisha mada, wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika katika Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa ufafanuzi wa hoja, wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kushoto), Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika katika Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini wakati wa kikao kazi kati yake na Watumishi wa Mkoa wa Simiyu kilichofanyika katika Shule ya Msingi Bariadi Alliance mkoani Simiyu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...