*Unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi. bilioni 10

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa mradi wa maji wa Kintiku – Lusilile ulioko Manyoni ambao awamu yake ya kwanza inatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba 22, mwaka huu.

Akizungumza na watumishi na wakadarasi leo (Ijumaa, Oktoba 4, 2019) mara baada ya kukagua mradi huo akiwa njiani kuelekea Manyoni, Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na ujenzi huo pamoja na kasi ya mkandarasi.

Waziri Mkuu ambaye ameanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Singida, alielezwa kwamba mradi huo utahudumia vijiji 11 vya Kintinku, Lusilile, Maweni, Mvumi, Ngaiti, Chikuyu, Mwiboo, Mbwasa, Mtiwe, Makutupora na Chilejeho ambavyo viko kando ya barabara kuu itokayo Singida kwenda Dodoma.

Akitoa taarifa ya mradi mbele ya Waziri Mkuu, Meneja wa RUWASA, Injinia Gabriel Ngongi alisema wananchi zaidi ya 55,000 watanufaika na mradi huo pindi utakapokamilika. Alisema awamu ya kwanza imegharimu sh. bilioni 2.46.

Akizungumzia halia halisi ya utekelezaji wa mradi huo, alisema ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji la lita 300,000 limekamilika lakini bado liko kwenye hatua ya umaliziaji. “Birika la kuhifadhia maji lemye ujazo wa lita milioni mbili limekamilika, bado shughuli za umaliziaji,” aliongeza.

Alisema ujenzi wa uzio, nyumba ya kuhifadhia mitambo na nyumba ya mlinzi umekamilika licha ya kuwa bado kuna kazi ndogo za umaliziaji.

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake wilayani Itigi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mkandarasi wa mradi wa maji Kintinku/Lusilile, Injinia Jumanne Werema, uliyopo katika Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida, Oktoba 4, 2019. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi. Waziri Mkuu yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku nne. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...