Charles James, Michuzi TV

ASASI 16 za Kiraia nchini zimetajwa kutoa mchango wa Bilioni 236 kwenye uchumi nchini ndani ya kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2016-2018.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze ambaye amesema licha ya kuwepo Asasi nyingi nchini lakini waliamua kufanya utafiti wa Asasi 16 tu ambazo zimefanyiwa uhakiki.

Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha mada ya mchango wa Azaki kwenye uchumi wa Nchi katika mkutano wa kwanza wa majadiliano ya Wiki ya Azaki jijini Dodoma 

Amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kilichopatikana kutokana na Asasi za kiraia kwa kipindi cha miaka mitatu ni sawa na kilo 2,181 za dhahabu zinazosafirishwa na kuuzwa nje ya Nchi.

“Lakini pia kiasi hicho cha fedha ambacho kimechangiwa na Asasi hizi 16, kwa kipindi hicho cha miaka mitatu ni sawa na serikali kuingiza watalii 42,316 na kukaa nchini kwa muda wa wiki moja au ni sawa lita 247 milioni za petrol,dezeli na mafuta ya taa” Amesema Eyakuze.

Pia Eyakuze amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu 2016/18 kiasi cha kodi ambazo zimelipwa na Azaki hizo 16 kwa serikali ni kiasi cha Sh. Bilioni 19.

Amefafanua kuwa kiasi hicho cha kodi kilichokusanywa kwa kipindi hicho ni sawa na mapato yatokanayo na maji ya kunywa, vinywaji laini na sigara ya mwaka 2018/19 ambayo yalikuwa ni bilioni 18.8.

“Au kiasi hicho cha kodi kilichokusanywa unaweza kulinganisha kabisa na kodi iliyokusanywa na Mamalaka ya maopato nchini TRA 2018/19 katika mikoa ya Rukwa, Lindi, Simiyu, Songwe na Katavi kwa pamoja ambayo makusayo yao ni Sh. Bilioni 21," Amesema Eyakuze.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society Francis Kiwanga, amesema katika wiki hiyo ya Azaki moja kati ya shuguli zitakazofanyika ni pamoja na kuwa na kongamano linalojumuisha wadau wengine ikiwemo serikali.

Amesema katika kongamano hilo wanajadiliana namna ya kushirikiana na kuweka mikakati ili mchango wa Asasi za kiraia uweze kutambulika na serikali.

Naye Mratibu wa Asasi za kiraia nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali a mitaa (Tamisemi) Denis Londo amesema Asasi la Kirai zinamchango mkubwa kwa Taifa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze akizungumza katika mkutano wa majadiliano wa wiki ya Azaki jijini Dodoma leo.
 Mratibu wa Asasi zisizo za kiserikali kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dennis Londo akizungumza wakati wa uchangiaji wa mada mbalimbali katika mkutano wa kwanza wa majadiliano wa wiki ya Azaki jijini Dodoma.
 Mmoja wa watoa mada wa mada ya haki na sheria akizungumza katika mkutano wa majadiliano kwenye ufunguzi wa wiki ya Azaki leo Dodoma.
Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali nchini waliojitokeza katika mkutano wa wiki ya Azaki inayoendelea jijini Dodoma. Asasi za Kiraia zipatazo 500 na Taasisi 100 zinashiriki mikutano hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...