Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akitambulisha
ujumbe alioambatanao kabla ya mazungumzo mafupi na na Mkuu wa Mkoa wa Manyara,
Mhe. Alexander Mnyeti alipomtembelea Ofisini kwake kabla ya kuendelea na ziara
yake ya kikazi Gereza Mbulu, leo Novemba 18, 2019. Mkuu huyo wa Jeshi la
Magereza amehitimisha ziara yake leo ya siku tatu Mkoani Manyara ambapo
ametembelea magereza na Kambi zote za magereza mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza na Mkuu wa
Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(hayupo pichani) alipotembelea
Ofisini kwake leo Novemba 18, 2019.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akiteta jambo
na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Alexander Mnyeti alipomtembelea Ofisi kwake
leo kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Gereza Mbulu, leo Novemba 18,
2019. 
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike akizungumza na
wafungwa na mahabusu wa Gereza Mbulu(hawapo pichani) leo Novemba 18, 2019 alipofanya
ziara ya kikazi katika gereza hilo(Picha zote na Jeshi la Magereza).
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini - CGP Phaustine Kasike(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Mbulu, SP. Danson Mpinga alipowasili Gereza Mbulu leo kwa ziara ya kikazi. Mkuu huyo wa Jeshi la Magereza amehitimisha ziara yake leo ya siku tatu Mkoani Manyara ambapo ametembelea magereza na Kambi zote za magereza mkoani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...