NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
WANANCHI wa Halmashauri ya Chalinze ,mkoani Pwani wameaswa kuendelea
kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kiweze kupete kwenye uchaguzi
mkuu ujao 2020 ,kutokana na utekelezaji madhubuti wa ilani ya Chama
Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake ,Dkt.John Magufuli kupunguza
changamoto katika sekta mbalimbali .
Akielezea namna utekelezaji wa ilani ya CCM ilivyogusa nafsi ya jamii
katika halmashauri hiyo, baada ya kikao cha baraza la madiwani
,Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu, alieleza
,maeneo yote ya jimbo hilo yamepita bila kupigwa kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa,vitongoji na vijiji hivyo anasema dalili ya mvua
mawingu anaimani CCM itashinda kwa kishindo 2020.
Zikatimu alisema, ndani ya miaka 57 jimbo hilo lilikuwa na nishati ya
umeme katika vijiji nane pekee ambapo tangu kuingia madarakani Rais
Magufuli zaidi ya vijiji 40 vina umeme na vingine vikiendelea
kufikishiwa umeme kupitia mradi wa REA ,Peri-Urban na ujazilizi.
Alibainisha, vijiji 20 ndivyo vilivyokuwa na maji ambapo kwa sasa
jumla ya vijiji 67 vinapata maji na mradi wa maji CHALIWASA unaendelea
hivyo kufikia mwaka ujao tatizo la maji litabaki historia.
Mwenyekiti huyo alielezea kwamba, zahanati 39 zilikuwepo na toka 2015
hadi sasa 43 zinajengwa na kati ya hizo nne zimekamilika,mbili zinatoa
huduma na nyingine zipo katika mbalimbali za ujenzi.
Aidha, katika kipindi cha July -Septemba mwaka huu jumla ya sh.milioni
416 zilitengwa kwa ajili ya mfuko wa vijana,wanawake na wenye ulemavu
.
"Wapinzani wanaona aibu, hawana jipya ,kwani Rais Magifuli kurejesha
heshima ya chama,ni mafanikio makubwa yametokana na utekelezaji wa
ilani na hakuna ubishi kwa hili"alifafanua Zikatimu.
Hata hivyo ,akizungumzia changamoto na mafanikio ya sekta ya
elimu,Zikatimu alisema halmashauri hiyo imetenga sh.milioni 360 kwa
ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na imetenga sh.milioni
579 kuzielekeza shule za sekondari kujenga madarasa.
"Sh.milioni 115 tumezipeleka Chahua kujenga shule mpya ya sekondari
ambazo zitasaidia kujenga madarasa sita,milioni 110 Lupungwi kata ya
Mandera kujenga madarasa matano na matundu ya vyoo,Pera milioni 40
kuongeza vyumba vy madarasa na milioni 60 kujenga maabara, na Kiwangwa
imepelekwa milioni 40"
Diwani wa kata ya Kimange,Hussein Hading'oka alisema shule ya
sekondari ya Kimange inakabiliwa na upungufu wa madarasa na bwalo la
kulia chakula wanafunzi kwani kwa sasa hamna hali inayosababisha kula
chakula chini ya miti.
Nae diwani kata ya Kibindu ,Ramadhani Mkufya alisema, katika kata hiyo
shule ya sekondari ina upungufu wa madarasa manne.
Alieleza, upungufu huo unasababisha msongamano madarasani ,kwani
wanafunzi wengine hukaa 150-200 katika darasa moja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...