*WANATAALUMA WAJADILI MIKAKATI YA
KUFIKIA UCHUMI WA KATI WA VIWANDA
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
kimefanya kumbukizi ya aliyekuwa Mkuu wa
chuo hicho Marehemu Profesa Joshua Doriye katika kutengamanisha utumishi wake pamoja taaluma ya utumishi wake uliotukuka .
Kumbukizi ya Profesa Doriye
kitaaluma kwa wanafamilia ya IFM katika kuenzi na kufuata utumishi wake
katika kufanya kazi sehemu mbalimbali kutokana na umahiri wake katika taaluma.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha Profesa Tadeo Satta amesema kuwa katika kuangalia
kumbukizi ya Profesa Doriye ni pamoja na
kuangalia taaluma katika kwenda katika uchumi wa viwanda kwa kufungua fursa ya wanafunzi wanaohitimu
kuingia katika uanzishaji wa viwanda.
Profesa Satta amesema serikali ya
awamu ya Tano imechukua wataalam wengi ili kuweza kusaidia na kushauri serikali kwenda katika mipango
yake ya kuipeleka Tanzania kwenda katika uchumi wa kati wenye viwanda.
Amesema kuwa wanafunzi wanaohitimu kwa sasa ndio wanaweza kufikisha mipango ya
serikali ya uchumi wa viwanda kwa kwenda na mawazo yao katika kufungua viwanda
na kuzalisha ajira zingine ambapo serikali itakuwa imepiga hatua ya maendeleo
inayoitaka.
Profesa Satta amesema kuwa kama
wataalam wanaangalia pamoja na kushirikiana na nchi ambazo zimepiga hatua za
kimaendeleo ikwemo India ambayo imepiga
hatua kutokana na sera walizozianzisha
zikazaa maendeleo.
Aidha amesema serikali imekuwa na
mikakati mbalimbali ikiwemo na ya kisera katika kuandaa wataalam kuwa
wazalishaji wa fursa za ajira kwa kuanzisha viwanda ambavyo vitazalisha ajira
kwa watu wengine.
Katika Kumbukizi ya Marehemu Profesa
Doriye mwenyekiti aliyeongoza majadiliano
ni Profesa Samuel Wangwe wa Daima Associate Limited na mwasilishaji mada Profesa Arunaditya Sahay
wa Taasisi ya Usimamizi wa Teknolojia ya Bibla nchini India.
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa
Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta akizungumza na waandishi habari katika kumbukizi
ya aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho Marrehemu Profesa Joshua Doriye iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
mwasilishaji mada wa Taasisi ya Usimamizi wa Teknolojia ya Bibla
nchini India Profesa Arunaditya Sahay
akitoa mada katika kumbukizi ya aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho Marrehemu Profesa
Joshua Doriye iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti majadiliano ni wa Daima
Associate Limited Profesa Samuel Wangwe akiendesha
majadiliano katika mada katika kumbukizi ya aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho
Marrehemu Profesa Joshua Doriye iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wanafunzi na IFM na wataalam wakiwa katika mada katika kumbukizi ya
aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho Marrehemu Profesa Joshua Doriye iliyofanyika
jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...