Na.Khadija Seif, Michuzi TV

MSANII wa Bongofleva Nasib Abdul a.k.a Diamond platinum amewapongeza wasanii,makampuni pamoja na vyombo vya habari kwa kufanikisha tamasha la wasafi lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Diamond amesema hayo katika ukumbi wa Hyatt regency uliopo jijini Dar es salaam ,nakugusia swala la wasanii hao kutoka nchi ya Nigeria kuwepo kwao kulikua na lengo maalumu.

"Lengo lilikua ni kujifunza kwa wenzetu jinsi ya kutumbuiza kwao kwa kuona mubashara tofauti na wengi wetu tulikua tunaona tu kupitia televisheni au kwenye mitandao ya kijamii,"

Aidha,mbali na kujifunza kutoka kwa wasanii hao wawili Diamond amefafanua zaidi kuwa wizkid na tiwasavage wataweza kututangaza kuanzia siku walipofika,sehemu watakazotembelea ,hivyo kutaleta ushawishi kwa watu ambao wanawatazama kutamani kufika nchi ya Tanzania.

Hata hivyo amewaomba wadhamini mwakani msimu mwingine wa Tamash hilo kuwaongezea fedha ili waweze kuwa na nafasi ya wasanii wengine kushiriki kikamilifu.

"Japo fedha ilikua pungufu sio sana lakini niliweza kutazama baadhi ya wasanii kwa jicho la kipekee kutokana na mara nyingi kutopewa nafasi kwenye majukwaa mbalimbali na ndio sababu pia sisi Kama wasafi na uongozi wa lebo yetu Wcb kuwapa nafasi wakongwe wa Muziki akiwemo inspector harun,Mandojo na domokaya,Madee na wengine kutumbuiza jukwaa la wasafi,"

Pia ametoa ushauri kwa wasanii kutosikiliza minong'ong'ono ya mashabiki zao wenye lengo la kuwagombanisha hasa mitandaoni.

"Wakati mwengine Mashabiki zetu wanatufanya tugombane ,tuchukiane na hata kutoelewana tuyapuuzie hayo kwani wote wanapenda kazi zetu kiujumla akitokea kwenye tamasha langu ataimba nyimbo zangu na akija kwako ataimba na zako huoni Kama wote Ni shabiki zetu tusiweke matabaka,"


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...