Na Woinde Shizza globu ya jamii ,Arusha

Kufuatia mkakati wa kuendelea kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu wa mitihani ya Taifa ya kidato cha nne, halmashauri ya Arusha imefanikiwa kupata chakula kwaajili ya wanafunzi wa kidato cha nne, katika kipindi chote cha mitihani ya Taifa inayotarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa wiki ijayo.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo wa chakula, kutoka Kanisa la Pentekoste- Ngulelo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Alvera Ndabagoye, licha ya kushukuru waumini wa kanisa hilo, amesema kuwa, uhakika wa uwepo wa chakula kwa wanafunzi, kipindi chote cha mtihani, utawawezesha wanafunzi, kutulia kisaikolojia na kufanya vizuri katika matokeo yao ya mitihani hiyo. 

Ameongeza kuwa, halmashauri inatambua na kuthamini mchango wa wadau wote, kutokana na uhalisia kuwa, Serikali peke yake haiwezi kutatua matatizo yote yanayoikabili sekta ya elimu, hivyo amewataka wadau kuendelea kujitoa kwa hali na mali kuunga mkono juhudi za aserikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Rais John Pombe Makufuli kwa kutoa elimu bila malipo.

Awali, Kiongozi wa Huduma ya Kanisa la Pentekoste Ngulelo, mwalimu Onesmo Anael, amesema kuwa, waumini wa kanisa lake, wameamua kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, kupitia Sera ya Elimu bila malipo na kuwa jukumu la chakula ni la wazazi, na kuamua kuwasaidia wazazi wasio na uwezo, kuwapa watoto hao chakula, kipindi chote cha kufanya mitihani ya Taifa mwaka 2019.

Amefafanua kuwa, wapo watoto yatima, wanaoshindwa kumudu kuchangia chakula shuleni, lakini pia wapo watoto ambao, wazazi wao hushindwa kuwachangia chakula cha mchana wawapo shuleni, kutokana na kipato chao kidogo, na kusababisha watoto wao kushinda bila kula wawapo shuleni.

"Kama kanisa, tumeguswa na hilo, tukaamua kuelekeza sadaka zetu, kwa wanafunzi wote wanaotegemea kuanza mitihani yao ya kidato cha nne wiki ijayo, kwa shule za ndani ya hamashauri yetu ya Arusha"alisema Onesmo.

Onesmo ameweka wazi kuwa, waumini wa kanisa lake, wamekusanya sadaka zao na kutoa jumla ya magunia 40 ya mahindi yenye kilo 100 na mifuko 20 ya maharage, kwa pamoja vikawasidie wanafunzi wetu wa kidato cha nne.

Naye Afisa Elimu Sekondari, Medard Lupenza, amethibitisha kuwa, kiasi hicho cha mahindi na maharagwe, kimegawanywa kwenye shule 26 za serikali zenye wanafunzi wa kidato cha nne, kwa uwiano kulingana na idadi ya wanafunzi.

Hata hivyo, wakuu wa shule zote 26, wamewashukuru uongozi wa kanisa la Pentekoste Ngulelo, pamoja na waumini wote, kwa kutambua na kuguswa na changamoto ya chakula, inayowakabili wanafunzi wasio na uwezo, na kuamua kujitoa kuchangia chakula ili kuwapa nafasi walimu na wanafunzi kufikiria mirihani tu.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa shule hao, Mwenyekiti wa Wakuu wa shule, Mwalimu Mwamvita Kilonzo, amesema kuwa walimu, hupata wakati mgumu sana pale ambapo, wazazi hushindwa kiwalipia watoto wao chakula, jambo ambalo husababisha unyonge kwa watoto wasiokula shuleni na kuwafanya hata walimu kujisikia vibaya.

Hata hivyo, mwalimu Kilonzo, amesema kuwa, uhakika wa uwepo wa chakula, utasababisha utulivu kwa walimu na wanafunzi, na kutegemea ufaulu kuongeza kwenye matokeo ya mtihani wa Taifa mwaka huu wa 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...