Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi ya Zanzibar, Mheshimiwa Assaa Ahmad Rashid akiongea katika kikao kifupi baina yake na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu walipokutana mapema leo Novemba 28, 2019 katika hoteli ya Madina Al Bahr iliyopo Visiwani Zanzibar. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu na Wa kwanza kulia ni Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo, Paul.
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi ya Zanzibar, Mheshimiwa Assaa Ahmad Rashid akiteta jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu walipokutana mapema leo Novemba 28, 2019 katika hoteli ya Madina Al Bahr iliyopo Visiwani Zanzibar.

Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi ya Zanzibar, Mheshimiwa Assaa Ahmad Rashid akiongozana kuelekea katika chumba cha mkutano na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu Novemba 28, 2019 katika hoteli ya Madina Al Bahr iliyopo Visiwani Zanzibar.

Picha ya pamoja.
Na
Mbaraka Kambona,
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu
ameitaja tasnia ya habari kuwa ndio wadau wakubwa wa haki za binadamu nchini.
Jaji
Mwaimu alitoa kauli hiyo Novemba 28, 2019 katika mkutano uliofanyika Visiwani
Zanzibar wa kuwajengea uelewa wa
pamoja Makamishna wa tume walioteuliwa
hivi karibuni na Rais John Magufuli.
Jaji
Mwaimu alieleza katika mkutano huo kuwa katika kutekeleza jukumu walilopewa la
kulinda, kuhifadhi na kutetea haki za binadamu chini wanawategemea sana vyombo
vya habari kuelimisha jamii kuhusu haki zao.
“Vyombo
vya habari ni wadau wetu wakubwa sana, wao ndio waelimishaji, wao ndio wamekuwa
wakati wote wakiibua matukio mbalimbali ya uvunjifu wa haki za binadamu kwa
lengo la kuujulisha au kuelimisha umma”,alisema Jaji Mwaimu
“Nyie
ndio mtakaoitangaza tume, kwa msingi huo, niseme kuwa tutaendelea
kuwashirikisha katika yale yote tutakayokuwa tunayafanya ili kupitia nyinyi
wananchi watafahamu kuhusu tume inachokifanya”,aliongeza
Mwenyekiti
huyo aliendelea kusema kuwa tume haiwezi kufanya kazi peke yake bila
kushirikiana na wadau wengine kama vyombo vya habari, Idara nyingine za
serikali, Asasi za Kiraia na taasisi za
kimataifa.
“Ni
lazima tujenge mahusiano mazuri ya kazi baina yetu, hatuwezi kufanya kazi peke
yetu, ni muhimu kufanya kazi na idara mbalimbali ikiwemo wadau wa maendeleo”,
alisisitiza
Naye,
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi ya Zanzibar, Assaa Ahmad Rashid, ambaye
ndiye aliyefungua mkutano huo kama mgeni rasmi, alimueleza Jaji Mwaimu kuwa
dhamana waliyopewa ni kubwa, kwa kuwa haki za binadamu ndio msingi katika nchi
yetu, wameaminiwa hivyo hawana budi kulitekeleza jukumu hilo kwa ufanisi mkubwa
ili kuwasaidia wananchi.
“Jukumu
mlilopewa Serikali ni kubwa, sisi tunawaahidi kuwa tutaendelea kutoa
ushirikiano katika kuifanya tume iweze kutekeleza majukumu yake vizuri”,
alisema Rashid
Rashid
aliendelea kusema kuwa Kuteuliwa kwa viongozi hao kunatoa fursa kamili na ya wazi kwa mwananchi kupeleka lalamiko lake, na
kwamba serikali imejenga mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa wadau wote
hususani Asasi za Kiraia, na wakati wote
serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote ikiwemo za kimataifa ili
kuhakikisha yale malengo yaliyowekwa yanafikiwa.
“Tunatambua
kuwa katika kutekeleza majukumu yenu kuna changamoto mnazo kutana nazo, ikiwemo
uelewa mdogo wa wananchi kuhusu haki zao,lakini muendelee kueneza elimu hiyo
kwa kushirikiana na taasisi zingine”,aliongeza Rashid.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...