Kugunduliwa kwa mafuta na gesi katika baadhi ya nchi za Afrika kumeweza kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kununua nishati nje kwa matumizi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa kipindi cha miaka 15, toka Tanzania ilipoanza kuzalisha na kusambaza gesi, imeokoa kiasi cha shilingi Trilioni 30, ambazo zingetumika kuagiza mafuta nje kwa ajili ya kuzalisha umeme na uendeshaji wa viwanda.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC James Mataragio, takriban asilimia 60 ya umeme unaozalishwa nchini unatumia gesi asilia, huku nishati hiyo pia ikitumika viwandani mbali na kutumika kuendesha magari katika siku za hivi karibuni.
Kulingana na Mwanahabari wa BBC Halima Nyanza magari yanayotumia mfumo wa gesi, yamekuwa yakiongezeka nchini Tanzania kila uchao.
Katika eneo la Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam, kunakopatikana kituo pekee kinachotumia mfumo wa gesi katika uendeshaji wa magari, Mwanahabari huyo alikutana na Augustin - dereva wa UBA, aalimwelezea ni nini haswa kilichomshinikiza kuanza kutumia mfumo wa gesi katika gari lake.
Dereva huyo anasema kwamba alilazimika kutumia nishati ya gesi kutokana na hali ngumu ya kiuchumi mbali na bei ya juu ya mafuta
''Ninatumia gesi kwa kuwa ni bei rahisi kulingana na hali ya uchumi ya sasa ilivyo, lakini pia ukitazama kuna tofauti kubwa sana ukilinganisha mafuta ambayo unaweza kutumia mengi kwa siku huku gesi ukitumia fedha chache lakini kwa muda mrefu''.
''Hii gesi nikijaza dola saba na Marekani in maana ninaweza kutembea kilomita 150 ukichanganya na foleni za mjini'', aliongezea.
PICHA KWA HISANI YA GETTY IMAGES

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC James Mataragio anasema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji vituo vingine viwili vikubwa vinatarajiwa kujengwa kwa ajili ya kusambaza gesi kwenye vituo vingine vidogo katika maeneo mbalimbali.
Bwana Mataragio anasema kwamba takriban magari 300 nchini Tanzania yamelkuwa yakitumia gesi badala ya mafuta , huku mengi zaidi yakiendelea kubadilishga mifumo yao ya mafuta hadi kuwa ile ya gesi
''Kufikia sasa zaidi ya magari 300 yanatumia gesi .Tulianza mwaka 2009 ambapo kituo cha kwanza cha gesi kilijengwa hapa Dar es salaam ambacho kinatumika katika kujaza magari gesi. Tangu kipindi hicho kumekuwa na karakarana ambazo zimekuwa zikibadilisha mifumo ya mafuta hadi gesi''.
kusoma zaidi bofya BBCSwahili.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...