Na Khadija seif, Michuzi TV

MUASISI wa jukwaa la wiki ya Maonesho ya mavazi Afrika Mashariki na kati Mustafa Hassanali ameweka wazi lengo lake la kukuza lugha ya kiswahili kupitia Sanaa ya ubunifu.

 Hassanali amesema hayo wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo la Maonesho la ubunifu wa mavazi( Swahili fashion week), ambapo kila mwaka huwakutanisha wabunifu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

"Mbali na kuonesha mavazi katika jukwaa hilo, kuna kuwepo na vitu vya kiubunifu vilivyobeba majina, kwa mfano mishono ya nguo ,Mwanamke nyonga,kibwaya ,mikufu,hereni ambavyo ni vya Kitanzania hivyo kwa namna moja au nyingine tunakua tumetangaza vitu vya kinyumbani zaidi kwa kupitia Sanaa ya ubunifu pamoja na lugha ya Kiswahili,"

Aidha jukwaa hilo la 12 tangu kuanzishwa kwake limepanga kufanyika desemba 6 hadi 8 katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam na litawakutanisha wabunifu 34 wa Afrika Mashariki na Ulimwenguni.

Hata hivyo Muasisi huyo amesema lengo la kuendeleza tasnia ya ubunifu Afrika bado linabaki mstari wa mbele kwa kupitia jukwaa Hilo na kwa Sasa wataweza kuona thamani ya bidhaa za ubunifu wa kitanzania na Afrika kwa ujumla.

Kwa upande wake Rais wa shirikisho la Sanaa za ubunifu na uchongaji (TAFCA) Adrian Nyangamale ameeleza kuwa jukwaa hili ni mojawapo ya njia ya kukuza vipaji vya wabunifu kwani inawashirikisha hata wale wanaochipukia.

"Watu wanakutana pamoja kutoka sehemu mbalimbali lakini hata wale chipukizi wanapewa nafasi ya kuonyesha ujuzi wao wakibunifu pia wanapata nafasi ya kuona wabunifu wakubwa nakujifunza vitu vingi ili kuboresha Sanaa zao"

Pia Nyangamale amesema mbali na kupewa fursa kwa chipukizi kuonyesha ubunifu wao ,fursa nyingine wanapatiwa wanamitindo kupita majukwaani hivyo kwa namna moja ama nyingine Mustafa ana unga Mkono Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya hapa kazi tu.

"Ni wachache wenye Moyo  wa kipekee na kujitolea kuwajengea uwezo na kuwapa moyo vijana ambao hawana ajira ila vipaji wanavyo na ndio maana hata katika swala la ubunifu wa mavazi Mustafa amechukua jukumu la kuwapatia ajira vijana wengi,"

 Hata hivyo Nyangamale ametoa wito kwa wadau, wabunifu na wapenzi wa ubunifu wa mavazi kutoa mchango wao,kuthamini na kuvipenda vya nyumbani ili kuendelea kujitangaza zaidi kimataifa kupitia mavazi y ubunifu.
Rais wa shirikisho la Sanaa za ubunifu na uchongaji akizungumza na waandishi wabunifu pamoja na waandishi wahabari wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Maonyesho la  ubunifu wa mavazi (Swahili fashion week) katika ukumbi wa Serena jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...