Na Ripota Wetu,Michuzi TV

KIJANA Mtanzania Erick Venant amepokea tuzo ya Legacy jijini London,ikiwa ni ya kutambua mchango wake katika kupambana na tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa(Antimicrobial resistance) na hasa kuongeza uelewa kwenye jamii na kutia hamasa ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya tatizo hilo.

Erick amepokea tuzo hiyo  Novemba 26 mwaka 2019, ambapo juhudi zake zinapaswa kuwa muhimu katika kuboresha afya ya ulimwengu. Akiwa Uingereza Erick amepata nafasi ya kukutana na Prince William katika makazi ya Kifalme, Kengstone palace ambapo walijadili kwa ufupi kuhusu tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa.

Kwa mujibu ya magazeti ya nchini Uingereza yameripoti jinsi Prince William alivyotumia lugha ya Kiswahili mara kadhaa wakati wa mazungumzo hayo.Erick ni miongoni mwa vijana 20 duniani waliochaguliwa kupokea tuzo ya Legacy waandaji wa tuzo hiyo "The Diana award" na kwamba inaelwzwa kwamba vijana wote waliochaguliwa wana mchango mkubwa kwenye jamii.

Washindi wengine wametoka mataifa ya Uingereza, Malaysia, India,Canada, Nigeria na Nepal.Mshauri mwandamizi wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Elizabeth Nyamayaro na mtendaji mkuu wa Shirika la ndege la Uingereza Alex Cruz ni miongoni mwa waliounda jopo la majaji 14 waliokutana kuchagua washindi 20 wa tuzo hii kutoka miongoni mwa washindi wa tuzo ya Diana award wa mwaka 2018 na 2019.

Sherehe za Utoaji wa tuzo zilifanyika katika ukumbi wa Old Royal Naval College,Greenwich-London na kuhudhuriwa na kaka mkubwa wa Princess Diana, Earl Spencer.Tuzo hii hufanyika kila baada ya miaka miwili.Tuzo za Diana award na Legacy award hutolewa kama kumbukumbu ya Princess Diana wa Wales aliyefariki mwaka 1997.Watu laki saba hufariki kila mwaka duniani kote kutokana na tatizo hilo.
 Kijana Erick Venant akiwa na tuzo yake  ya Legacy jijini London,chini Uingereza.
Kijana Mtanzania Erick Venant, akipongezwa na Prince William baada ya kukaribishwa kwenye makazi ya kifalme,Kingstone Palace kwa kupokea  tuzo ya Legacy jijini London,chini Uingereza.Tuzo hiyo imetolewa  Novemba 26,2019.
 Muonekano wa tuzo yenyewe.
 Picha ya pamoja na Wadau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...