Na Kijakazi Abdalla-Maelezo  
Kaimu Meneja Idara ya Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A) Mbarouk Khalid Ussi amesema kila mmoja ana wajibu wa kuisaidia Serikali katika ukusanyaji wa mapato.
Hayo ameyasema huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati  akifungua semina ya Wahasibu,Afisa Manunuzi pamoja na Wakaguzi wa hesabu wa taasisi za Serikali kuhusu kodi ya zuwio.
Amesema kuwa Serikali  inategemea kodi katika ukusanyaji wa mapato hivyo ipo haja kwa wafanyakazi hao  kusimamia na kutoa ushirikiano  ili kuhakikisha Serikali inapata mapato yao.
Amesema kuwa Serikali ina viazio vingi vya ukusanyaji wa  mapato hivyo ni vyema kuisaidia katika ukusanyaji kodi ili kuhakikisha lengo lilokusudiwa katika kuengeza pato la taifa linatimia
Nae Afisa Msimamizi wa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R .A) kwa upande wa Zanzibar Abdallah Seif Abdallah  amesema lengo la semina hiyo ni kuwakumbusha Wahasibu,Afisa Manunuzi pamoja na Wakaguzi wa Hesabu wa taasisi za Serikali  kujua wajibu wao wa  kuzuwia kodi ya zuwio ili kuongeza ukusanyaji wa mapato .
Aidha amewataka wafanyabiashara pamoja na watendaji hao kutoa mashirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A)  ili kuhakikisha hakuna upotevu katika ukusanyaji wa mapato na ulipaji wa kodi.
Akiwasilisha mada ya Kodi ya Zuwio kwa Wahasibu,Afisa Manunuzi pamoja na Wakaguzi wa Hesabu wa Taasisi za Serikali Afisa Mwandamizi Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa upande wa Zanzibar Shuweikha S.Khalfan amesema kuwa ni wajibu kwa wafanyakazi hao kujua sheria zote za walipa kodi.
 Kaimu Meneja Idara ya Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A) Mbarouk Khalid Ussi akifunguwa Mafunzo ya Kodi ya Zuwio kwa Wahasibu,Afisa Manunuzi na Wakaguzi wa hesabu kutoka Taasisi za Serikali huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
 Afisa Msimamizi wa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A) kwa upande wa Zanzibar Abdallah Seif Abdallah akitowa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa na Wahasibu,Afisa Manunuzi na Wakaguzi wa hesabu wa Taasisi za Serikali katika Semina inayozungumzia Kodi ya Zuwio huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
 Afisa Muandamizi Elimu na Huduma kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (T.R.A) Kwa upande wa Zanzibar Shuweikha .S. Khalfan akitoa mada kuhusu Kodi ya Zuwio kwa Wahasibu,Afisa Manunuzi na Wakaguzi wa hesabu wa Taasisi za Serikali katika Semina inayozunguzmzia  Kodi ya Zuwio huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Baadhi ya  Wahasibu,Afisa Manunuzi na Wakaguzi wa hesabu wa Taasisi za Serikali wakifatilia kwa makini  Semina inayozungumzia Kodi ya Zuwio huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.Picha na Maryama Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...