Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Klabu ya Soka ya Tottenham rasmi imemtaja Kocha raia wa Ureno, Jose Mourinho kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo baada yakumtimua aliyekuwa Kocha wake, raia wa Argentina Mauricio Pochettino.
Tottenham inakuwa timu ya tatu ya Uingereza kufundishwa na Kocha Mourinho baada ya awali kuzifundisha Manchester United na Chelsea.
Mourinho ametajwa kuwa Kocha wa Tottenham akichukua mikoba iliyoachwa na Kocha Mauricio Pochettino kwa kusaini kandarasi hadi mwisho wa msimu wa 2022-23.
Kupitia Tovuti ya BBC Sport, Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy amenukuliwa akisema kuwa “Kwa Jose tumepata Kocha mwenye mafanikio katika Soka na mwenye uzoefu kufundisha Soka”.
Baada yakutangazwa kuwa Kocha wa timu hiyo, Mourinho amesema “Navutiwa na ubora wa Kikosi chao kikubwa na Kituo chao cha Vijana (Academy). Kufanya kazi na Wachezaji wa Tottenham ni furaha kwangu”.
Mourinho akiwa Kocha nchini Uingereza alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu Soka nchini humo, Kombe la FA mara mbili akiwa na Chelsea, pia alishinda Europa League na Carabao Cup akiwa na Manchester United.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...