Dar es Salaam. Kampuni ya michezo kubashiri ya M-BET Tanzania imedhamini mashindano ya soka ya Ruvuma Vijana Cup ambayo yanashirikisha timu za wilaya zote sita za Mkoa wa Ruvuma.

Msemaji wa M-BET Tanzania, David Malley alisema kuwa kampuni yao imetoa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwa pamoja na Jezi na Mpira kwa timu mbalimbali zinazoshiriki katika mashindano hayo.

Malley alisema kuwa mbali ya jezi, soksi na mipira kwa timu , pia M-BET imedhamini vifaa vya mazoezi kama bips.

Alisema kuwa jezi hizo zitagawiwa kwa timu zitakazofuzu hatua ya 16 bora ya mashindano ambapo fainali yake itafanyika Desemba 15 kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Sokoine.

“Huu ni mwendelezo wa mchango wa kampuni yetu katika kuendeleza michezo, tulianza na KMC ambayo tumeidhamini kwa Sh 1 billioni kwa miaka mitano,” alisema Malley.

Kwa upande wake, mratibu wa mashindano hayo, Raymund Mhenga alisema kuwa mashindano hayo yalishirikisha jumla ya timu 32 ambapo sasa yapo katika hatua ya mtoani kuelekea hatua ya 16 bora.

“Tunawashukuru M-BET Tanzania kwa msaada huu ambao utahamasisha maendeleo ya soka mkoani Ruvuma ambapo mwaka jana, wachezaji 10 walisajiliwa na timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Majimaji,” alisema Mhenga.

Mhenga alisema kuwa mashindano hayo yanazidi kushika kasi na mipango yao ni kuyafanya kuwa ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Alisema kuwa mipango yao ni kuziharika timu za Yanga na KMC kushuhudia mashindano hayo ili kusaka vipaji kama ilivyokuwa kwa Majimaji.
 
Msemaji wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET, David Malley (kulia) akimkabidhi mpira mratibu wa mashindano ya Ruvuma Vijana Cup, Raymund Mhenga baada ya kampuni hiyo kutangaza kudhamini mashindano hayo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...